RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


JINSI ya kupata Birth Certificate Online

Filed in Makala by on 15/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

JINSI ya kupata Birth Certificate Online

JINSI ya kupata Birth Certificate Online,RITA Online Birth certificate Verification, RITA Online Birth, Certificate Login, Birth certificate Tanzania, RITA Online Registration, RITA birth certificate, Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Online.

JINSI ya kupata Birth Certificate Online

JINSI ya kupata Birth Certificate Online,RITA Online Birth certificate Verification, RITA Online Birth, Certificate Login, Birth certificate Tanzania, RITA Online Registration, RITA birth certificate, Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Online.

Kuzaliwa na Kifo – Tovuti ya Mtandaoni TARATIBU ZA KUPATA HUDUMA ZA KUZALIWA NA KUFA.

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) unapenda kuufahamisha Umma kwamba, sasa watu wanaweza kutumia huduma zetu hapa chini kupitia mtandao:

  1. Maombi mapya ya usajili wa Vizazi na Vifo.
  2. Uhakiki wa cheti cha Kuzaliwa na Kifo.

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuomba:

  1. Hifadhi maelezo uliyotumia kuunda akaunti.
  2. Mwombaji lazima awe na taarifa zake sahihi pamoja na wazazi wote wawili.
  3. Mwombaji atapata bili/namba ya Udhibiti na atatakiwa kulipa kupitia Benki (NMB na CRDB) au Huduma za Malipo ya Simu (M-PESA, TIGO PESA na AIRTEL Money) kwa mujibu wa taarifa ulizopewa.
  4. Mwombaji awe na nakala laini za viambatisho vinavyohitajika katika muundo wa pdf.
  5. Mwombaji kutaja wilaya ya mahali pa kuchukua cheti.

Aidha, tunapenda kuwasihi waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu.

Viungo vya maombi pamoja na Mwongozo wa Maombi vinapatikana chini ya ukurasa huu.

Kumbuka: maombi hayatashughulikiwa kabla ya kukamilisha malipo ya huduma. Kwa maelezo zaidi piga 0800 117 482

MFUMO WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO

Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya cheti cha kuzaliwa au kifo kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote.

Baada ya kujaza fomu ya maombi ya cheti cha kuzaliwa au kifo, atatakiwa kuichapisha (Print) na kuiwasilisha
pamoja na vielelezo vingine katika Ofisi ya Wilaya iliyo karibu naye kwa ajili ya
kushughulikiwa maombi yake ya Cheti.

VIELELEZO VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU YA MAOMBI YA CHETI CHA KUZALIWA.

  • Tangazo la kizazi kwa vizazi vilivyosajiliwa ndani ya muda katika vituo vya tiba
  • Kadi ya Kliniki
  • Cheti cha ubatizo
  • Pasi ya kusafiria
  • Cheti cha kumaliza elimu ya msingi au secondari (leaving certificate)
  • Kitambulisho cha Utaifa au Kadi ya kupigia kura
  • Vitambulisho vya Utaifa au Kadi ya kupigia kura vya wazazi
  • Picha ya Mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light blue Background)
  • Zingatia/Muhimu Mwombaji lazima aambatishe vielelezo si chini ya viwili kati ya hivyo vilivyotajwa
    pamoja na vitambulisho vya wazazi.
JINSI ya kupata Birth Certificate Online,RITA Online Birth certificate Verification, RITA Online Birth, Certificate Login, Birth certificate Tanzania, RITA Online Registration, RITA birth certificate, Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Online.

JINSI ya kupata Birth Certificate Online

VIELELEZO VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU YA MAOMBI YA CHETI CHA KIFO

Tangazo la kifo kwa kifo kilichoandikishwa ndani ya muda katika kituo cha tiba Kwa kifo kilichotokea nyumbani au kuchelewa kuandikishwa mwombaji aambatishe

BARUA YA UTAMBULISHO: Mwombaji wa cheti cha kifo kilichochelewa
kuandikishwa anatakiwa kuleta barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa
Mtendaji wa Kata/kijiji wa eneo tukio lilipotokea.

Barua hiyo inatakiwa itaje majina kamili ya marehemu, tarehe ya kifo, mahali alipofia na sababu za kifo.

Vilevile picha ndogo ya Mwombaji iweke kwenye barua hiyo na igongwe muhuri.

MUHTASARI WA KIKAO CHA WANANDUGU:

  • Ndugu wa marehemu wanatakiwa wakae kikao na kuandaa muhtasari ambao una agenda za kikao ambazo pamoja na mambo mengine ni kumteua msimamizi wa mirathi ambaye ndiye atakayetambulika kisheria kufuatilia cheti cha kifo.
  • Kikao kihudhuriwe na ndugu wa marehemu.
  • Pia watatakiwa kuorodhesha majina yao na kuonyesha uhusiano wao na marehemu.
  • Ndugu hao watatakiwa waweke sahihi kuthibitisha ushiriki wao.
  • Muhtasari huu uthibitishwe na Afisa Mtendaji wa Kata/kijiji kwa kugonwa muhuri nakuweka sahihi yake.

ANGALIZO:

  • Ifahamike kuwa muhtasari huo unatakiwa ushirikishe ndugu
    wote wa karibu wa marehemu ili kuondoa migogoro inayoweza kutokea.
  • Pia endapo Msajili atakuwa na mashaka juu ya yaliyomo katika muhtasari huo anaweza kuwaita baadhi ya waliohudhuria kwa mahojiano zaidi.

HATI YA KIAPO: Hati ya kiapo kutoka mahakamani au kwa mwanasheria
iliyoapiwa na mwombaji (Msimamizi wa Mirathi) na kueleza taarifa za marehemu kama majina kamili, tarehe ya kifo na mahali alipofia na sababu za kifo Uhakiki wa Vyeti vya Vizazi na Vifo

Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kuwasilisha maombi ya kuhakiki cheti ha kuzaliwa na kifo kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote.

Muombaji atatakiwa kuscan cheti cha kuzaliwa au kifo anachohitaji kihakikiwe na kisha kukituma kwa njia ya kieletroniki ili kihakikiwe.

Majibu ya uhakiki yatatumwa katika akaunti uliyofungua sehemu iliyoandikwa ‘’View Status” Linki ya kuingia katika mfumo: https://online.rita.go.tz

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , , , , , , , , , , ,

Comments are closed.