JOHN Bocco Atambulishwa JKT Tanzania FC
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JOHN Bocco Atambulishwa JKT Tanzania FC
JOHN Bocco Atambulishwa JKT Tanzania FC, Klabu ya JKT Tanzania FC imekamilisha usajili wa Nahodha wa zamani wa Klabu ya Simba, John Raphael Bocco kama Kocha Mchezaji.
Bocco alitangaza kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuitumikia Simba kwa misimu saba.
Klabu yake ya Simba ilimuunga mkono katika uamuzi huo huku ikichukua jukumu la kumpeleka kusomea mafunzo ya ukocha aliyoanza tangu mwezi Machi mwaka huu na wakati huohuo akipewa jukumu la kukinoa kikosi cha Simba U17.
Hata hivyo Bocco amesitisha mpango wake wa kustaafu akipewa mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya JKT Tanzania FC.
Bocco amesajiliwa kama mchezaji lakini pia atatumika kama mmoja wa makocha katika benchi la ufundi la timu hiyo.