JOHN Bocco Kuangwa Simba Day 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JOHN Bocco Kuangwa Simba Day 2024
JOHN Bocco Kuangwa Simba Day 2024, Pamoja na Simba kutangaza kuachana na John Bocco baada ya mkataba wake kumalizika, imejulika nahodha huyo wa zamani ataagwa katika Tamasha la Simba Day.
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema kuwa Bocco atapewa mwaliko maalum katika Simba Day ili apate nafasi kuagwa rasmi na klabu, Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo.
Hata hivyo Ahmed amesema kuwa Bocco ataendelea kuwa Mwanafamilia wa Simba ambapo klabu itaendelea kumuunga mkono katika majukumu yake ya ukocha mpaka pale mwenyewe atakavyoamua vinginevyo.
“Kawaida ya Simba ni kuheshimu mchango wa wachezaji wake wote. John Bocco tunatambua mchango wake na tutasimama naye mpaka pale yeye mwenyewe akisema inatosha kwa kuwa ni familia yetu na atabaki kuwa kwenye familia.
“Unaona kuna mchezaji Mussa Mgosi yeye alicheza Simba na sasa anafundisha kwenye timu ya wanawake hata Suleiman Matola naye alicheza Simba kwa sasa anaifundisha Simba hivyo ni mwendelezo wetu kusimama na wachezaji wetu kila wakati.”
Ni wazi kwamba Bocco kwenye Ligi Kuu Bara anashikilia rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 100 akiwa ni mzawa mwenye uwezo mkubwa kwenye eneo la Ushambuliaji kwa miaka ya hivi karibuni.
Bocco alijiunga Simba msimu wa 2017/18 akitokea Azam FC na kutoka hapo amekuwa muhimili wa timu ndani na nje ya uwanja.
Bocco amekuwa msaada mkubwa kwa wachezaji vijana pamoja na wale wageni waliokuwa wakija kikosini hapo na alikuwa kiunganishi bora kati ya Uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.
Katika kipindi cha miaka saba Bocco aliyodumu kikosini ameiongoza timu hiyo kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu mfululizo, Kombe la FA pamoja na Kombe la Mapinduzi.