JOSEPH Guede kumpisha Sowah Yanga
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JOSEPH Guede kumpisha Sowah Yanga
JOSEPH Guede kumpisha Sowah Yanga, Klabu ya Yanga ipo kwenye Mazungumzo ya kumpata Mshambuliaji raia wa Ghana, Jonathan Sowah kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Al-Nasr Benghazi ya Libya aliyojiunga nayo Januari 2024 kwa Mkataba wa miaka miwili akitoka Medeama ya kwao.
Taarifa zinadai kuwa endapo dili lake litakamilika, uwezekano wa Yanga kuachana na Joseph Guede aliyejiunga na Yanga Januari 2024 akitokea Tuzlaspor FC ya Uturuki ni mkubwa. Lakini hata Kennedy Musonda na yeye huenda akapigwa chini muda wowote.
Sowah anakumbukwa zaidi wakati alipokutana na Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi ambapo alifunga bao moja pindi timu hizo zilipofungana 1-1, December 8, 2023 kisha kwenye marudiano ambapo Medeama kuchapwa 3-0.
Sowah aliwasumbua sana Yanga kwenye mechi hiyo, hatua ambayo iliwafanya Yanga kuendelea kumfuatilia zaidi ingawa baadae wakapunguza kasi baada ya kusajiliwa na timu ya Al-Nasr Benghazi ya Libya Katika dirisha dogo la Usajili.
Tangu ajiunge na Al-Nasr Benghazi dirisha dogo Sowah ameifungia mabao matano ambapo mchezo ambao aling’aa ni ule dhidi ya Al Hilal Benghaz aliofunga mabao manne peke yake wakati timu yake ikishinda 6-3.