JOSHUA Mutale ni Mnyama
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JOSHUA Mutale ni Mnyama
JOSHUA Mutale ni Mnyama, Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji, Joshua Mutale raia wa Zambia Kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Power Dynamos ya kwao Zambia.
Mutale mwenye miaka 22 anamudu kucheza nafasi nyingi Uwanjani tena kwa ufanisi wa hali ya juu.
Joshua anaweza kumudu nafasi ya winga ya kulia, kushoto na wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji yaani namba 10.
Akiwa Power Dynamos msimu uliopita, Mutale amefunga mabao matano na kuisaidia kupatikana kwa mengine matatu katika michezo 26 alizocheza.
Uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi nyingi Uwanjani pamoja na umri ni miongoni mwa vigezo ambavyo Simba imevitumia kumsajili mchezaji huyo ikiwa ni mkakati maalumu wa kuboresha kikosi chake kwa kusajili damu changa na wenye ubora.
Joshua Mutale anakua ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Simba baada ya Lameck Lawi kutoka Coastal Union FC ya Tanga.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: JOSHUA Mutale ni Mnyama