Joshua Mutale nje ya dimba wiki mbili
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Joshua Mutale anatarajiwa kuwa nje ya dimba takribani wiki mbili baada ya kuchanika nyama za paja.
Kwamba huyo za Zambia alipata majeraha hayo katika mchezo wa kwanza wa Ligi kuu dhidi ya Tabora United uliopigwa Jumapili iliyopita, kwenye uwanja KMC Compex, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Taarifa hizo zimethibitishwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally Kwa kusema kuwa Mutale hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Fountain Gate katika mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Jumapili ya August 25-2024.
“Ni kweli Mutale alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Tabora United, hayakuwa majeraha makubwa sana lakini jambo la uhakika tutamkosa katika mchezo wetu unaofuata dhidi ya Fountain Gate,” alisema Ahmed
Taarifa ya kitabibu kutoka kwa daktari wa Simba, Edwin Kagabo baada uchunguzi wa jeraha la Mutale, imebainisha kuwa nyota huyo hakupata majeraha makubwa lakini wameona ni vyema apumzishwe kwa wiki mbili ili awe amepoma vyema.