JOYCE Lomalisa Apewa Thank You
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
JOYCE Lomalisa Apewa Thank You
JOYCE Lomalisa Apewa Thank You,beki wa kushoto raia wa DR Congo, Joyce Lomalisa Mutambala hatokuwa sehemu ya kikosi cha Young Africans SC kwa msimu ujao wa 2024-2025.
Hiyo ni baada ya mkataba wake wa miaka miwili alioutumikia kumalizika mwisho wa msimu wa 2023/2024.
Ikumbukwe kuwa beki huyo alijiunga na Young Africans mwanzoni mwa msimu wa 2022/2023 na kushiriki katika mafanikio yaliyopatikana misimu miwili mfululizo.
Ndani ya Young Africans, Lomalisa ameshinda Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC mara mbili mfululizo kama ilivyo katika Kombe la FA, pia taji moja la Ngao ya Jamii.
Pia amekuwa sehemu ya kikosi cha Young Africans SC kilichocheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022/2023 na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/2024.