KANUNI zinaibeba Simba Kesi ya Lawi na Coastal Union
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
KANUNI zinaibeba Simba Kesi ya Lawi na Coastal Union
KANUNI zinaibeba Simba Kesi ya Lawi na Coastal Union,Wakili Nduruma Majembe, amesema kuwa shauri la Simba lililopelekwa kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuhusu kuvunjiwa Mkataba na Coastal Union wa kumsajili beki Lameck Lawi, imeonekana timu hiyo haikuwa na mamlaka hayo kwani walipaswa kupelekwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini ambao ndiyo wenye mamlaja ya kutafsiri sheria.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu sakata hilo ambalo lilizungumzwa juzi kwenye Ofisi za TFF, Nduruma, alisema wanaamini Coastal haikufanya sahihi, kwani wao hawana uwezo huo, bali wangelipeleka kwenye vyombo maalum na si wao kuamua kuhusu suala la mchezaji huyo.
Simba ilimsajili Lawi ambaye ni beki wa kati na ilipomtangaza tu, viongozi wa Coastal Union waliibuka na kudai kuwa klabu hiyo ilikiuka makubaliano ambayo ni ya kulipa pesa kabla ya siku ya mwisho iliyoainishwa ndani ya mkataba.
Alisema mkataba wa mpira, kuna vitu vikifanyika haviwezi kupanguka kwa mujibu wa Kanuni za CAF na Fifa, ambapo mkataba ukiingiwa utakuwa tayari umeshakamilika, na malipo yana eneo lake.
“Huu si kama mkataba wa kuuziana kuku au mbuzi ambapo usipoleta pesa kesho basi unavunjika, haipo hivyo, mikataba ya mpira wa miguu ina taratibu zake.
Kama mtu hajalipa kwa siku 30 ndipo inapokuwa tatizo, na hata hivyo ni lazima uandike notisi, na baada ya hapo siku 10 baada ya kupewa ndipo klabu inatakiwa ikamilishe malipo hizo ndizo taratibu zilivyo,” alisema wakili huyo ambaye aliwahi kuisimamia kesi ya Bernald Morrison dhidi ya Klabu ya Yanga miaka kadhaa nyuma.
Alisema hoja iliyopo mezani ni Coastal kusitisha mkataba wa Lawi kuichezea Simba kama ni halali au la.
“Sidhani kwamba Coastal walilalamika kutambulishwa, ila ni kwamba pesa ya klabu ilipaswa kulipwa kufikia Mei 31, na wakati huo ligi ilikuwa bado inaendelea, wakati wanasainiana ilikubaliwa ligi ikiisha wampeleke kufanyiwa vipimo, malalamiko yao ni kwamba Simba walichelewesha malipo zaidi ya tarehe hiyo, yalifanyika Juni 10.
“Simba wao walisema walichelewa kwa sababu walikuwa wanasubiri wamfanyie vipimo, ikiwa ni moja kati ya matekelezo ya kimkataba, haikuwezekana kwa sababu aliitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, lakini baadaye Simba walilipa bila hilo kutekelezeka,” alisema na kuongeza;
“Ushahidi unaonyesha kuwa mpaka Juni 3, Simba na Coastal walikuwa wanaendelea na mazungumzo. Ilipolipwa, tarehe 17, wakaandika barua ya kusitisha mkataba ikiwa ni siku 10 baada ya kupokea pesa yote.”
Akabainisha Coastal hawakufanya vyote hivyo ambavyo walitakiwa kuvifanya, na hata kama ingekuwa vinginevyo, walipaswa kupeleka shauri TFF kwenye kamati husika na si kumzuia mchezaji na kudai kuvunja mkataba, kitu ambacho hawana mamlaka nacho.