KAULI ya Fadlu Davids kuelekea mchezo vs Yanga Ngao ya Jamii 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
KAULI ya Fadlu Davids kuelekea mchezo vs Yanga Ngao ya Jamii 2024
KAULI ya Fadlu Davids kuelekea mchezo vs Yanga Ngao ya Jamii 2024, Kocha Mkuu Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa pamoja nakuwa wamepata wiki tatu za maandalizi kuelekea msimu ujao wa ligi lakini wanahitaji kupata ushindi katika mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Kocha huyo amesema kuwa Simba imesajili wachezaji wapya 14 ambao wengi wao ni vijana huku wapinzani wal wakiwa pamoja kwa muda mrefu lakini hilo haliwasumbui na wapo tayari kwaajili ya kupambana.
Aidha kocha Fadlu ameongeza kuwa kwenye kikosi chake kina aina tofauti za wachezaji kulingana na mpinzani wanayekutana naye kwahiyo wapo tayari kuwakabili Yanga.
“Mchezo wa Kesho utatupa mwanga kuelekea msimu ujao wa Ligi, utatuonyesha maandalizi yetu ya wiki tatu kule Misri yalikuwa bora au la.
“Hatuna presha tutaingia kwenye mchezo wa kesho kama ilivyo kwenye mechi nyingine lakini tumejipanga kupata ushindi,” amesema Kocha Fadlu.
Kwa upande wake Nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ yeye amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwaajili ya mchezo huo na watafanyia kazi maagizo watajayopewa na walimu.
“Maandalizi yetu yamekamilika, sisi kama wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na walimu wetu lakini lengo letu ni kushinda,” amesema Zimbwe Jr.