KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

KAULI ya Matola Kuelekea mchezo vs Yanga April 20-2024

Filed in Michezo by on 19/04/2024 0 Comments

KAULI ya Matola Kuelekea mchezo vs Yanga April 20-2024

KAULI ya Matola Kuelekea mchezo vs Yanga April 20-2024

KAULI ya Matola Kuelekea mchezo vs Yanga April 20-2024

KAULI ya Matola Kuelekea mchezo vs Yanga April 20-2024, Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema kuwa wako tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho Jumamosi April 20 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Matola amesema kuwa wamekuwa na wakati mzuri wa kujiandaa na mchezo huo, ari na morali ya Wachezaji ikiwa juu

“Tumekuwa na wakati mzuri wa kujiandaa na mchezo huu. Tunafahamu tunakwenda kucheza dhidi ya timu nzuri. Yanga wamekuwa bora na mwendelezo mzuri wa matokeo katika mechi zao”

“Lakini niseme tu, tumejiandaa vyema na tuko tayari kukabiliana nao na lengo letu ni kupata ushindi,” alisema Matola

Aidha Matola amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kesho ili kuwaongezea hamasa wachezaji wao huku akiahidi watafurahi

“Niwaombe mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuongeza hamasa kwa wachezaji”

“Hii ni mechi mpya, tumeandaa mkakati tofauti wa kuicheza mechi hii, niwahakikishie watafurahi”

Aidha Matola amesema kuwa bado wako katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu na wanafahamu ni lazima washinde mchezo wa kesho ili kuendelea kubaki katika mbio hizo

Akizungumza kwa niaba ya Wachezaji wenzake, nahodha Msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe amesema kuwa wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo.

Kapombe pia amesema kuwa wamekuwa na wakati mzuri wa maandalizi ambapo amebainisha kuwa kocha Abdelhak Benchikha amefanya kazi kubwa kuhakikisha wanakuwa tayari kwa mchezo huo

“Sisi kama wachezaji tuko tayari kupambana, tutahakikisha tunacheza vizuri na kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kesho dhidi ya Yanga”

“Mwalimu amepata nafasi kubwa ya kuiandaa timu na kutuandaa sisi katika nyanja zote, hivyo niseme tuko tayari kwa ajili ya kuipambania klabu ya Simba,” alisema Kapombe

Kupitia Nijuze Habari utaweza kufuatilia Update zote za mchezo huo, dakika baada ya dakika hadi dakika 90 ukobofya hapa.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *