KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

KAYMZIWANDA amtaka Mo Dewji aondoke Simba!

Filed in Michezo by on 23/04/2024 0 Comments

KAYMZIWANDA amtaka Mo Dewji aondoke Simba!

KAYMZIWANDA amtaka Mo Dewji aondoke Simba!

KAYMZIWANDA amtaka Mo Dewji aondoke Simba!

KAYMZIWANDA amtaka Mo Dewji aondoke Simba!, Shabiki  na Mwanachama wa Klabu ya Simba, Kaymziwanda amesema kuwa kama Tajiri wao anapata hasara aondoke tu.

Kay amesema hayo baada ya Simba kuzorota na kushindwa kupata matokeo kwa michezo minne mfululizo ikiwemo kichapo cha bao 2-1 walichopokea juzi dhidi ya watani zao Yanga.

“Haya tuanzie hapa bwana tajiri kwanza tunashukuru kwa mchango wako mkubwa sana ndani ya miaka 4 hilo kila Mwanasimba atakupongeza. Turudi ndani ya misimu hii mitatu Simba imesajili wachezaji wengi ambao kiukweli aina ya wachezaji na malengo ya timu ni vitu viwili tofauti.

“Swali kwako bwana tajiri je, unatoa hela za usajili? Na kama unatoa hao ndo aina ya wachezaji uliowataka? Kama ndio uliwataka unawekaje malengo makubwa wakati unasajili wachezaji wa kawaida ambao kihalisia hawawezi kufikia malengo ya timu?

“Na kama sio je, wewe kama mtu unaetoa fedha za usajili unaridhikaje na aina ya watu kama hao wanao kuletea wachezaji tena sio mara moja ni zaidi ya misimu 3, nini ulikiamua ukiwa kama tajiri.

“Kila siku umekuwa ukisema Simba inakupa hasara sasa tajiri kama kitu kinakupa harasa why usiachane nacho ukakaa pembeni? Halafu ukaona kama hii Simba itakufa au itapotea.

“Mara oooh tutasajili mchezaji yoyote Africa, sikia bwana tajiri mpira ni mchezo wa wazi na ni biashara pia, leo tunavaa jezi zilizo jaa matangazo yako unasemaje unapata hasara?

“Kama mpaka leo bado upo Simba basi kwa namna moja ama nyengine Simba inakufaidisha bwana Tajiri, achana na kujisifu sana insta mara umefanya hivi mara vile, acha mameno mengi Tajiri toa pesa timu isajili.

“Simba ina malengo makubwa sana na wewe unajua tumechoka huu usajili wa Instagram kila mwaka weka pesa bwana timu ilete watu wa maana Mo Dewji hii Simba sio mali ya mtu ni timu ya wanachama,” amesema Kaymziwanda.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *