KHOMEINY Aboubakar Khomeiny ni Mwananchi
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
KHOMEINY Aboubakar Khomeiny ni Mwananchi
KHOMEINY Aboubakar Khomeiny ni Mwananchi,Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa golikipa, Khomeiny Aboubakar Khomeiny Kutoka Singida Black Stars zamani Ihefu FC.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25, anakuja kuungana na Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery katika kulinda lango la Klabu hiyo.
Ujio wa Khomeiny ni sehemu ya
kuboresha kikosi Cha Yanga kuelekea msimu ujao ambapo uwepo wake utaongeza kitu cha tofauti Klabuni hapo.
Yanga imefikia hatua hiyo ya kumsajili Khomeiny kutokana na uzoefu wake na msingi bora wa kisoka alionao kutokana na kucheza timu zote za taifa za Tanzania za vijana ikiwemo U-20 na U-23.
Khomeiny anakuwa mchezaji wa nne mpya Kusajiliwa na Young Africans SC baada ya kiungo Clatous Chama Kutoka Simba SC, Mshambuliaji Prince Dube Kutoka Azam FC, na beki wa kushoto Chadrack Boka Kutoka Eloi Lupopo ya nchini DR Congo.