RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


KIKOSI Cha Tanzania Kilichoitwa vs Zambia Kufuzu Kombe la Dunia

Filed in Michezo by on 27/05/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

KIKOSI Cha Tanzania Kilichoitwa vs Zambia Kufuzu Kombe la Dunia

KIKOSI Cha Tanzania Kilichoitwa vs Zambia Kufuzu Kombe la Dunia

KIKOSI Cha Tanzania Kilichoitwa vs Zambia Kufuzu Kombe la Dunia

KIKOSI Cha Tanzania Kilichoitwa vs Zambia Kufuzu Kombe la Duniaz Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Suleiman ‘Morocco’ ameita jumla ya Wachezaji 34 wanaounda Kikosi Cha Tanzania kitakachoingia Kambini Kujiandaa na mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia.

Aidha, Morocco ameendelea kutomuita beki wa Yanga, Dickson Job baada ya kutofautiana naye wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast mapema mwaka huu kufuatia mchezaji huyo kukataa kucheza beki ya kulia akisistiza apangwe katikati.

Aidha Tanzania imepangwa pamoja na Morocco, Zambia, Niger, Kongo na Eritrea ambayo imejitoa katika Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.

Taifa Stars ilianza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger November 18 mwaka jana Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao pekee la Mshambuliaji Charles William M’Mombwa wa Macarthur FC ya Australia.

Taifa Stars inatarajiwa kushuka Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola kumenyana na Zambia katika mchezo wake wa Pili wa kufuzu Kombe la Dunia.

KIKOSI Kamili Cha Tanzania Kilichoitwa vs Zambia Kufuzu Kombe la Dunia

MAKIPA
1:Ally Salim – Simba SC.
2: Abutwalib Mshery – Young Africans.
3:Kwesi Kawawa – Syrianska FC, Sweden.
4:Yonna Geoffrey – Tanzania Prisons.

MABEKI
5:Haji Mnoga – Aldershot Town, England.
6:Bakari Mwamnyeto – Young Africans.
7:Ibrahim Abdallah – Young Africans.
8:Nickson Kibabage – Young Africans.
9:Mohamed Hussein – Simba SC.
10:Lameck Lawi – Coastal Union FC.
11:Israel Mwenda – Simba SC.
12:Mukrin Issa – Ihefu FC.
13:Lusajo Mwaikenda – Azam FC.
14: Pascal Msindo – Azam FC.
15:Nathaniel Chilambo – Azam FC.

VIUNGO
16:Novatus Dismas – Shakhtar Donestsk, Ukraine.
17: Yusufu Kagoma – Singida Fountain Gate.
18:Morice Michael – RFK Novi Sad, Serbia.
19:Himid Mao – Tala’ea El Gaish SC, Egypt.
20:Mudathir Yahya – Young Africans.
21:Feisal Salum – Azam FC.
22:Yahya Zaydi – Azam FC.
23:Abel Josiah – TDS (TFF Academy)

WASHAMBULIAJI
24:Edwin Balua – Simba SC.
25:Simon Msuva – Alnajmah FC, Saudi Arabia.
26:Kibu Denis – Simba SC.
27:Cpyrian Kachwele – Whitecaps FC 2, USA.
28:Ben Starkie – Likeston Town, England.
29:Charles M’mombwa – Marcathur FC, Australia.
30:Waziri Junior – KMC FC.
31: Ibrahim Hamad – Zimamoto FC.
32:Kelvin Pius John – KRC Genk, Belgium.
33:Clement Mzize – Young Africans.
34: Abdul Suleiman – Azam FC.

Wachezaji wa Young Africans na Azam FC watajiunga na timu baada ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la TFF Maarufu CRDB Bank Federation Cup itakayofanyika June 02 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Mcongo man says:

    Mmmh kikosi kizur shida ni kujitoa tu kizalendo