KOCHA Fadlu Davids Kuelekea Mchezo vs APR FC Simba Day 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
KOCHA Fadlu Davids Kuelekea Mchezo vs APR FC Simba Day 2024
KOCHA Fadlu Davids Kuelekea Mchezo vs APR FC Simba Day 2024,Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa mchezo wa kesho dhidi ya APR wa kilele cha Simba Day utakuwa mzuri ambao utampa picha kuelekea msimu ujao wa mashindano wa 2024/2025.
Kocha Fadlu amesema kuwa litakuwa jambo zuri kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho kutokana na kuwa na sherehe lakini atawapa nafasi wachezaji wote ili kuzoea mazingira ya kucheza katika wingi wa mashabiki.
Aidha Kocha, Fadlu ameupongeza Uongozi wa klabu hiyo kwa kusajili wachezaji bora wenye umri mdogo ambao wana nguvu na ari ya kuipambania Simba kufikia malengo yaliyowekwa.
“Kikosi kipo kwenye hali nzuri, mchezo wa kesho utakuwa kipimo bora kwetu, tunafahamu mashabiki watajitokeza kwa wingi uwanjani nasi tunaona itakuwa jambo zuri kuwapa furaha ya ushindi.”
“Ninafahamu Simba haijatwaa taji la ligi kwa miaka mitatu lakini safari hii tuna timu bora ambayo najivunia kuwa itatupeleka kwenye malengo tuliyojiwekea,” amesema Kocha Fadlu.
Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo, Mohamed Hussein amewatoa hofu Wanasimba na kuwaambia kuwa wana timu imara ya ushindani na kesho wataanza kupata furaha waliyokuwa wanaisubiri.
“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua kuwa ni sikukuu ya Wanasimba na tiketi zimeisha siku tatu kabla kwahiyo wachezaji tunajua tuna jambo kubwa la kufanya,” amesema Zimbwe Jr.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: KOCHA Fadlu Davids Kuelekea Mchezo vs APR FC Simba Day 2024