LEONEL Ateba Kutua Simba SC
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
LEONEL Ateba Kutua Simba SC
LEONEL Ateba Kutua Simba SC, Klabu ya Simba SC ipo Katika hatua za mwisho kukamilisha usajili Mshambuliaji wa kati, Leonel Ateba raia wa Cameroon Kutoka USM Alger ya Algeria.
Kwa sasa, Simba na USMA wanaendelea na mazungumzo kuhusu ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Lionel Ateba aliwahi kucheza kwenye Vilabu vya Coton Sport, PWD Bamenda na Dyn. Douala pia alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 27 wa Cameroon kwaajili ya AFCON 2023.
Aidha Simba imelazimika kurudi sokoni haraka kutafuta mshambuliaji mwingine kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumpa nguvu Mshambuliaji Steve Mukwala.
Mwingine anayetajwa kusakwa na Simba ni Mshambuliaji, Elvis Kamsoba raia wa Burundi ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kuachana na Perserikatan Sepakbola Sleman ya Indonesia.
Kamsoba mwenye miaka 28, amewahi kuvichezea vilabu vya mbalimbali zikiwemo Melbourne Victory FC na Sydney FC za Australia.
ikiwa mmoja kati yao atajiunga na klabu hiyo itabidi Klabu ipunguze mchezaji mmoja wa kigeni ili kuendana na idadi ya wachezaji 12 wanaohitajika kikanuni.
Nyota ambao wanaweza kuondolewa ndani ya Simba ni mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Freddy Michael Kouablan aliyejiunga na Simba January 2024 akitokea Green Eagles ya Zambia, akiwa amefunga mabao sita ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Mwingine ni kipa Ayoub Lakred licha ya kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja lakini anaweza kuachwa baada ya ujio wa kipa raia Guinea, Moussa Camara aliyetoka Horoya AC ya Guinea.
Ukiachana na wawili hao, mwingine anayeweza kuachwa ili kupisha usajili wa mshambuliaji mpya ni kiungo, Fabrice Ngoma ambaye inaelezwa yupo tayari kuondoka ndani ya timu hiyo huku akiwa na ofa kutoka Libya.
Msako huo wa mshambuliaji mpya unakuja baada ya benchi la ufundi chini ya Kocha, Fadlu Davids kutoridhishwa na uwezo wa Mganda, Steven Dese Mukwala aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Asante Kotoko ya Ghana.