Leonel Ateba ruksa kutumika Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Mshambuliaji mpya wa Klabu ya Simba SC, Leonel Ateba tayari amepata vibali vitakavyomuwezesha kuitumikia Simba katika mechi zinazofuata.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha kuwa tayari uongozi wa klabu hiyo umekamilisha taratibu zote za vibali kwaajili ya mshambuliaji huyo.
Kutokana na taarifa hiyo, mchezaji huyo anaweza kuonekana katika mchezo wa Ligi Kuu utakaofuata dhidi ya Fountain Gate Jumapili ya August 25-2024 saa 10:00 jioni.
“Tayari uongozi umekamilisha taratibu zote za vibali vya mshambuliaji wetu mpya Ateba, yaani yuko tayari na wanasimba wanaweza kumuona uwanjani katika mchezo unaofuata dhidi ya Fountain Gate,“alisema Ahmed
Aidha Ahmed amethibitisha Simba kuachana na mshambuliaji, Freddy Michael baada ya kutomridhisha kocha mkuu, Fadlu Davies.
“Mwalimu Fadlu hakuridhika na kiwango cha Freddy. amefanya jitihada za kumuimarisha katika kiwanja cha mazoezi ili aendane na falsafa yake lakini pale iliposhindikana ndio akaomba aletewe mshambuliaji mwingine na uongozi ukamletea mashine ya kupatwa kwa jua, Leonel Ateba,” alisema