LEY Matampi Kipa Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
LEY Matampi Kipa Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
LEY Matampi Kipa Bora Ligi Kuu ya NBC 2023/2024,Golikipa wa Coastal Union ya Tanga, Ley Matampi ameibuka Kipa Bora wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kumaliza na Clean sheets 15, moja zaidi ya Djigui Diarra wa Young Africans.
Matampi aliyempiku Djigui Diarra wa Yanga ambaye huu ni msimu wake wa tatu, tayari ameshinda tuzo hiyo misimu miwili mfululizo akimshusha Aishi Manula wa Simba aliyewahi kujiwekea utawala wake kwa misimu sita mfululizo tangu akiwa Azam FC kabla ya kuhamia Simba 2017.
Matampi huu ni msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na Coastal Union akitokea Jeunesse Sportive Groupe Bazan ya kwao DR Congo.
Matampi amecheza mechi 24 kati ya 30 za Ligi Kuu, sawa na dakika 2160 na kumzidi Djigui Diarra wa Yanga ambaye amecheza mechi 21 kati ya 30 akifikisha jumla ya dakika 1846 na jumla ya clean sheet 14.
Makipa wote hao wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu zao kwa msimu huu kwani Diarra ameiwezesha Yanga kutetea taji lake la Ligi Kuu, huku Matampi akiiwezesha Coastal Union kumaliza nafasi ya nne na kufuzu kucheza Kombe la Shirikisho msimu ujao wa 2024/2025.
Coastal imepata nafasi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989 iliposhiriki Kombe la Washindi Afrika na kuishia raundi ya kwanza.
Baada ya hapo ndipo michuano hiyo ilikuja kuunganishwa na Kombe la CAF na kuzaliwa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2004.