RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

Filed in Michezo by on 09/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

Na Mariam Kagenda – Kagera

LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

Wizara ya utamaduni,sanaa na michezo nchini tayari imeanza hatua ya kutafuta vipaji kupitia michezo mbalimbali inayoendelea zikiwemo ndondo Cup ili kukuza vipaji ajira,ushirikiano pamoja na mahusiano.

Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni,sanaa na Michezo Hamis Mwijuma amesema hayo julai 06,2024 wakati akizindua Ligi ya Byabato Cup ya Mbunge wa Jimbo la Mjini Wakili, Stephen Byabato Mkoani Kagera ambapo amesema Serikali ya awamu ya sita kwa inatambua umuhimu wa michezo ikiwa ni njia moja wapo ya kuboresha afya na kuoneka kama kazi nyingine maana vijana wengi wameajiriwa katika sekta za burudani na michezo kupitia hapo wemekuwa matajiri wakubwa jambo ambalo linakuza uchumi na maendeleo ya Nchi.

LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo“Mhe. Rais ametupatia kazi hiyo ya kusaka vipaji kote nchini niwahakikishie kwenye ligi hii nitaleta skauti hapa ili kuangalia vijana wenye vipaji na tuhakikishe tunawapeleka kwenye timu kubwa waweze kuhudumia nchi hii”amesema Naibu waziri Mwijuma.

Katika hatua nyingine Naibu waziri Mwijuma amesema mwaka 2027 Tanzania inaandaa mashindano ya AFCON kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunafanya marekebisho makubwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, Amani na tunajenga uwanja wa Samia Suluhu Hassan Arusha huku tutaendelea kufanya marekebisho katika viwanja mbalimbali na mchakato huo utafika kaitaba stadium kwa juhudi za Mhe, Rais Samia.

Ligi ya Byabato Cup imeanza kutimua vumbi julai 06 mwaka 2024 ikishirikisha timu 14 za kata zote ambapo mechi ya awali ilikutanisha timu za wanawake Victoria Queen’s dhidi ya Omiseta Queen’s mpaka dakika tisini zinatamatika za muamuzi wa kati Geturuda Gerevazi zimetoka sale ya goli mbili na Mchezo wa ufunguzi wa jioni umekutanisha timu ya Bilele na Bakoba.

LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na MichezoKwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini wakili, Stephen Byabato amemshukuru Naibu waziri wa Utamaduni ,Sanaa na Michezo Hamis Mwijuma kwa kuzindua ligi hiyo ambayo itakuwa msaada mkubwa wa kichocheo cha michezo kwa wakazi wa Bukoba.

Amesema kuwa yeye kama kiongozi anatambua umuhimu wa michezo kwa kukuza vipaji na upande wa ajira pia ndo maana ameamua kuweka ligi hiyo na kuongeza kuwa ataendelea kuwasaidia vijana kuinua vipaji vyao .

Katika ligi hiyo ya Byabato Bukoba Cup mshindi wa kwanza atapata kiasi cha shilingi Milioni 3, wa pili Milioni 2 na wa 3 Milioni 1

LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

LIGI ya Byabato Bukoba Cup Yazinduliwa Rasmi na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: ,

Comments are closed.