LUIS Miquissone apewa Thank You Simba
LUIS Miquissone apewa Thank You Simba
LUIS Miquissone apewa Thank You Simba,Simba yaachana na Luis Jose Miquissone, Simba yamuacha Miquissone, Luis Miquissone aachana na Simba, Simba yaachana na Miquissone 2024.
Klabu ya Simba imefikia maamuzi ya kutomuongezea Mkataba Kiungo mshambuliaji, Luis Jose Miquissone baada ya mkataba wake kumalizika.
Miquissone aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezeka kama kiwango chake kitaridhisha lakini kutokana kiwango duni alichoonesha klabu imeamua kutomuongezea mkataba mwingine.
Miquissone alijiunga Simba kwa mara ya kwanza Januari 2020 akitokea UD Songo ya Msumbiji ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka Mamelodi Sundowns na katika kipindi hicho alionyesha uwezo mkubwa na kuibuka kipenzi cha Wanasimba.
Julai 22 mwaka jana Miquissone alirejea tena Simba kutoka Al Ahly ambapo aliuzwa na Simba lakini hata hivyo makali yake hayakuweza kuwa kama ya awali hivyo Uongozi umeamua kutomuongezea mkataba mpya.
Tangu amejiunga Simba msimu huu amecheza mechi 19 za ligi kuu ya NBC akitoa assist tatu na kufunga bao moja pekee katika mashindano ya Mapinduzi.
Uongozi umedhamiria kufanya maboresho makubwa ya kikosi kuelekea msimu ujao wa Ligi na Miquissone hayupo kwenye mipango ya timu hiyo.
Simba imemtakia kila la kheri katika maisha mapya ya soka nje ya timu hiyo.
Tags: Luis Miquissone aachana na Simba, LUIS Miquissone apewa Thank You Simba, Simba yaachana na Luis Jose Miquissone, Simba yaachana na Miquissone 2024., Simba yamuacha Miquissone