MAJINA 4582 ya Walioitwa kwenye Usaili UTUMISHI June 02-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MAJINA 4582 ya Walioitwa kwenye Usaili UTUMISHI June 02-2024
MAJINA 4582 ya Walioitwa kwenye Usaili UTUMISHI June 02-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Leo June 02-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Taasisi Mbalimbali za UMMA Leo June 02-2024, TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 02-06-2024.
- NAFASI za Kazi kutoka Shirika la Uvuvi TAFICO June 02-2024
- MAJINA ya Walioitwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT 2024
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali (GCLA), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kampuni ya Magazeti
ya Serikali (TSN), Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Wizara ya Kilimo, Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) anapenda kuwataarifu
Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 08-06-2024 hadi
21-06-2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka
Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka. - Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
Mwombaji. - Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA) - Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
- Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili
- Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
RATIBA YA USAILI WA MCHUJO NA VITENDO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA 4582 YA WALIOITWA KWENYE USAILI TAASISI MBALI ZA UMMA LEO JUNE 02-2024
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: MAJINA 4582 ya Walioitwa kwenye Usaili UTUMISHI June 02-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Taasisi Mbalimbali za UMMA Leo June 02-2024, Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Leo June 02-2024, TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 02-06-2024.
Usaili wa jeshi la polisi2024 unafanyika lini: