MAJINA 901 ya Walioitwa kwenye Usaili Kinondoni March 2024
MAJINA 901 ya Walioitwa kwenye Usaili Kinondoni March 2024
MAJINA 901 ya Walioitwa kwenye Usaili Kinondoni March 2024, MAJINA 901 ya Walioitwa kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni 11-03-2024,Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni 11-03-2024, Kuitwa Kwenye Usaili Kinondoni Municipal 2024.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni anapenda kuwatangazia waombaji kazi wa Kada ya Dereva Daraja la II, Afisa TEHAMA Daraja II na Afisa TEHAMA Msaidizi kwamba wafuatao wametimiza sifa elekezwa hivyo wafike katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani iliyopo Kata ya Ndugumbi, Mtaa wa Makanya siku ya Jumamosi tarehe 16/03/2024 kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Wasailiwa wote wafike na vyeti halisi (Original Certificates) pamoja na nakala ya vyeti husika siku ya usaili kama ifuatavyo:-
- Cheti cha Kidato cha Nne
- Vyeti vya Ujuzi (Professional)
- Cheti cha Kuzaliwa
- Kitambulisho cha Uraia/Mpiga Kura
- Leseni kwa Madereva
MAJINA 901 ya Walioitwa kwenye Usaili Kinondoni March 2024
Orodha ya walioitwa kwenye usahili imeambatanishwa kwenye PDF Bofya hapa Kudownload
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ni moja kati ya Halmashauri tano (5) zinazounda Mkoa wa Dar es Salaam. Zingine ni Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Ubungo, Kigamboni na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilianzishwa kwa Sheria ya Serikali (Mamlaka za Miji) sura ya 288 kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice No. 4) ya mwaka 2000 na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kama chombo huru, hivyo kuipa mamlaka ya kuongeza ubora wa utoaji huduma kwa wananchi wake.
1.2 MIPAKA YA ENEO
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inapakana na Bahari ya Hindi kwa upande wa Mashariki, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa upande wa Kusini, Wilaya ya Bagamoyo kwa upande wa Kaskazini na Wilaya ya Ubungo kwa upande wa Magharibi. Halmashauri inaunganishwa na sehemu nyingine za miji na nchi kwa mtandao wa barabara za mawasiliano. Barabara kuu ni pamoja na barabara ya Morogoro, Bagamoyo, Kawawa, barabara ya Sam Nujoma, Mwai Kibaki na Ally Hassan Mwinyi.
1.3 HALI YA HEWA:
Hali ya hewa ya Manispaa ya Kinondoni ni ya joto la wastani wa nyuzi joto 290C kwa mwaka. Kipindi cha joto huanzia kati ya miezi ya Oktoba hadi Machi, wakati kipindi cha baridi chenye kadirio la nyuzi joto 250C huanzia kati ya miezi ya Mei hadi Agosti na nyuzi joto 29 – 330C kwa miezi iliyosalia katika kipindi cha mwaka. Wastani wa mvua kwa mwaka ni mm 1,300 katika misimu miwili ambayo ni vuli miezi ya Oktoba – Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi – Mei.
1.4 ENEO NA IDADI YA WATU
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ina ukubwa wa kilomita za mraba 321. Kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya idadi ya watu na makazi ya mwaka 2012, Manispaa ya Kinondoni ilikuwa na idadi ya watu wapatao 929,681. Kutokana na ongezeko la ukuaji wa idadi ya watu ya asilimia 5.0 kwa mwaka, Manispaa inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 1,373,562 ifikapo mwaka 2020, hivyo kila kilometa ya mraba kuwa na ujazo wa watu 4,279.
1.5 UTAWALA
Kiutawala Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imegawanyika katika Tarafa mbili (2) ambazo ni Kinondoni na Kawe, Kata ishirini (20) na Mitaa ni mia moja na sita (106) ya utawala. Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi ni mawili (2) ambayo ni Majimbo ya Kinondoni na Kawe. Mkuu wa Wilaya ni Msimamizi Mkuu wa shughuli zote za Serikali katika Wilaya. Manispaa inaongozwa na Baraza la Madiwani lenye wajumbe ishirini na tisa (29) ambapo kuna Madiwani 26 na Wabunge 3 ambapo Mstahiki Meya ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Manispaa ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa.
1.6 MAJUKUMU YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI
Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:-
- Kuimarisha na kuwezesha amani, maagizo na utawala bora ndani ya eneo la utawala wake.
- Kuweka msisitizo kwenye shughuli za ustawi wa kijamii na kiuchumi kwa watu wote waliopo ndani ya eneo la Halmashauri kulingana na Mipango na Sera ya Taifa kwa maendeleo ya Halmashauri, Halmashauri ina jukumu la kuendeleza maendeleo katika nyanja za kijamii na kiuchumi ndani ya eneo la Halmashauri.
- Kuweka msisitizo na kuhakikisha ushirikishwaji wa kidemokrasia katika kutoa maagizo yanayohusu watu wenyewe.
- Kuanzisha na kuimarisha vyanzo madhubuti vya mapato na vyanzo vingine ili kuwezesha Serikali za Mitaa kutekeleza kazi nyingine kikamilifu.
- Kusimamia ujenzi wa miundombinu ya barabara, majengo, umeme na maji.
- Kuimarisha na kuendeleza shughuli za biashara, viwanda, masoko na sekta zisizo rasmi.
- Kutoa huduma za afya tiba, kinga na uboreshaji wa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii.
- Usafi na udhibiti wa taka ngumu na maji taka katika eneo la Halmashauri.
- Kusimamia na kutoa elimu ya Msingi na Sekondari katika eneo la Halmashauri.
- Kusimamia na kuratibu mapambano ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI na kudhibiti maambukizi mapya.
- Kusimamia utekelezaji Sera, Sheria za nchi na Sheria ndogo za Halmashauri.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania March 06-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Kuitwa Kwenye Usaili Kinondoni Municipal 2024., MAJINA 901 ya Walioitwa kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni 11-03-2024, MAJINA 901 ya Walioitwa kwenye Usaili Kinondoni March 2024, Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni 11-03-2024