RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MAJINA ya Waliochaguliwa Ajira za NEC 2024

Filed in New by on 18/07/2024

MAJINA ya Waliochaguliwa Ajira za NEC 2024

MAJINA ya Waliochaguliwa Ajira za NEC 2024, NEC Selected Applicants NEC Jobs 2024, Majina ya waliochaguliwa Ajira za NEC 2024, Orodha ya Majina ya Waliotwa Kazini NEC 2024, Orodha ya Majina ya Waliopangiwa vituo vya Kazi NEC 2024, Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Ajira za NEC 2024, Nafasi za kazi nec 2024,NEC Tanzania, Kirefu cha nec, Mwenyekiti wa NEC,NEC Tanzania address, Tume ya taifa ya uchaguzi tanzania nec,Katibu wa nec, Who is the current chairperson of NEC in Tanzania,NEC verification Tume ya taifa ya uchaguzi in english,Jinsi ya kupata namba za kitambulisho cha mpiga kura,Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi.

MAJINA ya Waliochaguliwa Ajira za NEC 2024

MAJINA ya Waliochaguliwa Ajira za NEC 2024, NEC Selected Applicants NEC Jobs 2024, Majina ya waliochaguliwa Ajira za NEC 2024, Orodha ya Majina ya Waliotwa Kazini NEC 2024, Orodha ya Majina ya Waliopangiwa vituo vya Kazi NEC 2024, Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Ajira za NEC 2024.


Historia ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

KUASISIWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Mwaka 1991 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi aliteua Tume ya kwanza chini ya Uenyekiti wa Marehemu Jaji Mkuu Mstaafu Francis Nyalali Madhumuni ya Tume hii ilikuwa kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuendelea na mfumo wa chama kimoja au kuwa na mfumo wa vyama vingi.

Kutokana na ushauri wa Tume ya Nyalali ,Sura ya 3 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ilirekebishwa na kufanya Tanzania kuwa Taifa linalofuata mfumo wa Vyama vingi vya Siasa.

Sheria ya Vyama vya siasa, (Na. 5ya 1992) ilirekebishwa ili kuwezesha kuandikishwa kwa vyama vya siasa. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,(Na.1ya 1985), Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,(Na. 4 ya 1979) na sheria zinazoendana pia zilirekebishwa ili kuondokana na matakwa ya chama kimoja na kuruhusu mchakato wa Kufanyika kwa Uchaguzi chini ya Mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Mwaka1993 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa chini ya Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Wajumbe wa Tume waliteuliwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 January 1993.

KUUNDWA KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Na Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaundwa na wajumbe wafuatao:-

  1. Mwenyekiti ambaye ni lazima awe amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania au mwanasheria mwenye sifa za kuwa wakili na ambaye amekuwa katika wadhifa huo si chini ya miaka 15
  1. Makamu mwenyekiti ambaye ni lazima awe amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania au mwanasheria mwenye sifa za kuwa wakili na ambaye amekuwa katika wadhifa huo si chini ya miaka 15.

iii. Mjumbe aliyeteuliwa kutoka kaika chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society).

  1. Wajumbe wengine wanneni watu ambao wana uzoefu katika kuendesha na kusimamia chaguzi au sifa nyingine za ziada ambazo Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataona zinafaa.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 1 ya1985), Mkurugenzi wa Uchaguzi ndiye Katibu wa Tume ambaye pia huteuliwa na Rais.

Mzunguko wa Uchaguzi

MZUNGUKO WA UCHAGUZI TANZANIA

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 65 inaelekeza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ufanyike kila baada ya kipindi cha miaka mitano (5). Kama ilivyo kwa Nchi nyingine Duniani, katika kuendesha shughuli za Uchaguzi, Tanzania hutumia utaratibu wa mzunguko wa Uchaguzi ambao shughuli zake hugawanywa katika awamu tatu (3). Awamu hizo ni shughuli kabla, wakati na baada ya Uchaguzi.

Hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza mfumo wa mzunguko wa Uchaguzi kwa kufuata awamu hizo Tatu kama ifuatavyo:

(a) Kabla ya Uchaguzi

Shughuli zilizofanyika katika awamu kabla ya Uchaguzi ni pamoja na:

(i) Uandaaji wa Bajeti;

(ii) Uandikishaji wa Wapiga Kura;

(iii) Ununuzi wa Vifaa;

(iv) Uandaaji wa Kalenda na Mpango wa Utekelezaji;

(v) Marekebisho ya Sheria na Maelekezo ya Watendaji na Wadau wa Uchaguzi;

(vi) Mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi;

(vii) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura; na

(b) Wakati wa Uchaguzi

Katika awamu hii, Tume ilifanya shughuli zifuatazo:

(i) Uteuzi wa Wagombea;

(ii) Uratibu wa Kampeni za Wagombea.

(iii) Utekelezaji wa Kamati za Maadili;

(iv) Usajili wa Watazamaji wa Uchaguzi.

(v) Kuchapa na kusambaza Karatasi za Kura;

(vi) Kusambaza Vifaa vya Uchaguzi;Upigaji Kura;

(vii) Kuhesabu Kura; na

(viii) Kutangaza Matokeo.

(c) Baada ya Uchaguzi

Katika awamu hii, Tume inafanya shughuli zifuatazo:

(i) Tathmini baada ya Uchaguzi Mkuu;

(ii) Kushughulikia Kesi za Uchaguzi; na

(iii) Kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu.

(iv) Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi;

(v) Kupitia na kuboresha Daftari la Wapiga Kura;

(vi) Kupitia na kuboresha Mifumo ya Uchaguzi;

(vii) Kupitia na kuboresha mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi;

(viii) Kupitia na kuboresha Muundo wa Tume;

(ix) Ukaguzi wa matumizi ya fedha na vifaa vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu;

(x) Kupitia Mpango Mkakati; na

(xi) Kuandaa Mpango Kazi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaofuata. Bofya Hapa.

Mfumo wa Uchaguzi

Mfumo wa Uchaguzi Tanzania

Mfumo wa Uchaguzi Tanzania ni kuwa anayepata kura nyingi ndiye mshindi. Hii inamaanisha kuwa Rais, Mbunge au Diwani atakayepata kura nyingi ndie atakayetangazwa mshindi. Aidha kuna uwakilishiwa Viti Maalum kwa wabunge na madiwani kwa uwiano wanaopewa wanawake kulingana na kura halali ambazo chama kimepata.

MUUNDO WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Tume inaundwa na Wajumbe saba (7), miongoni mwao wakiwemo Mwenyekiti na

Makamu Mwenyekiti ambao wanapaswa kuwa na sifa ya Jaji wa Mahakama Kuu au

Mahakama ya Rufani. Katika Uteuzi, Rais anazingatia kuwa endapo Mwenyekiti ni

mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu

anayetoka sehemu ya pili ya Muungano. Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) na (2)

ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na Kifungu cha

4(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Aidha, Mjumbe mmoja anateuliwa kutoka miongoni mwa Wanachama wa Chama cha

Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society – TLS) na Wajumbe wengine

wanne (4) wanatakiwa wawe na uelewa wa kutosha kuhusiana na kusimamia na

kuendesha Uchaguzi wa Wabunge au sifa nyingine kama ambavyo Rais wa Jamhuri

ya Muungano atakavyoona inafaa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Tume.

Tume ina jumla ya Wajumbe saba (7), kama inavyoonesha hapa chini:-

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Na. Jina Wadhifa

  1. Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele, Mwenyekiti
  2. Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk, Makamu Mweyekiti
  3. Mhe. Jaji Asina Abdillah Omari, Mjumbe
  4. Mhe. Balozi Omar Ramadhani Mapuri, Mjumbe
  5. Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira, Mjumbe
  6. Mhe. Jaji Rufaa Mwanaisha Athuman Kwariko, Mjumbe
  7. Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar, Mjumbe

Wajumbe wa Tume hukaa Madarakani kwa kipindi cha miaka mitano tangu

kuteuliwa kwao, lakini Rais anaweza kuwateua tena kwa kipindi kingine kadri

atakavyoona inafaa.

Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume husaidiwa na Sekretarieti

inayoongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye ndiye Mtendaji Mkuu na Katibu

wa Tume. Kwa sasa Mkurugenzi wa Uchaguzi ni Ndugu Kailima, R.K.

Aidha, Tume ina Idara 6, Ofisi ya Zanzibar na Vitengo 3 kama ifuatavyo:-

(i) Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi;

Majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi

(ii) Idara ya Daftari na TEHAMA;

Majukumu ya Idara ya Daftari na TEHAMA

(iii) Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura;

Majukumu ya Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura

(iv) Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu;

Majukumu ya Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu

(v) Idara ya Mipango Ufuatiliaji na Tathmini;

Majukumu ya Idara ya Mipango Ufuatiliaji na Tathmini

(vi) Idara ya Usimamizi wa Manunuzi na Lojistiki;

Majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Manunuzi na Lojistiki

(vii) Kitengo cha Huduma za Sheria

Majukumu ya Kitengo cha Huduma za Sheria

(viii) Ofisi ya Zanzibar;

Majukumu ya Ofisi ya Zanzibar

(ix) Kitengo cha Fedha na Uhasibu; na

Majukumu ya Kitengo cha Fedha na Uhasibu; na

(x) Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani;

Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Tags: , , , , , , , , , , , , , , ,

Comments (2)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Majina ya walio chaguliwa NEC wilaya ya chamwino

  2. Majina ayo yako wapi?