MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 2024
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 2024,Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngara 20-07-2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara anawatangazia wafuatao kuwa wanatakiwa kuhudhuria usaili wa maandishi na mahojiano ya ana kwa ana ajira za mkataba kwa nafasi zifuatazo,
- Mratibu wa LADP(LADP Tanzania Coordinator)
- Afisa Manunuzi (LADP Tanzania Procurement Officer) na
- Afisa Mazingira (LADP Environmental Expert).
Tanzania
Wasailiwa waliokidhi vigezo na kuitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika tarehe 25/07/2024 hadi tarehe 26/07/2024 kama ilivyoainishwa kwenye ratiba kamili ya usaili.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika na kitambulisho kwaajili ya utambuzi.
- Vitambulisho vitakavyokubalika ni pamoja na kitambulisho cha mpiga kura, kitambulisho cha makazi, kitambulisho cha Taifa (NIDA) au hati ya kusafiria.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti halisi (original) ambavyo ni:- Cheti cha kuzaliwa, Cheti cha kidato cha IVVI, Shahada kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la awali la ajira.
- Aidha testmonials, Provisional results, statement of results, Hati ya matokeo ya kidato cha IV/VI havitakubaliwa na wahusika hao hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha usaili.
- Pia kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU/NACTE).
- Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Kila msailiwa azingatie tarehe ya usaili na muda.
- Usaili utafanyika katika ukumbi wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Mkabala na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuanzia saa 2:00 asubuhi.
- Matumizi ya simu hayataruhusiwa kwenye chumba cha usaili.
- Waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.
- Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakaopotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
Aidha, ratiba ya usaili pamoja na majina ya waombaji waliokidhi vigezo kwa nafasi mbalimbali zilizotangazwa imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini!
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA KUITWA KWENYE USAILI NGARA DC
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Wilaya ya Ngara July 2024, Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngara 20-07-2024.