MAJUKUMU na Kazi za Mwenyekiti wa Kijiji
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MAJUKUMU na Kazi za Mwenyekiti wa Kijiji
MAJUKUMU na Kazi za Mwenyekiti wa Kijiji, Majukumu ya Mwenyekiti wa Kijiji, Kazi za Mwenyekiti wa Kijiji, Majukumu na Kazi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri Mbalimbali Tanzania.
- MAJUKUMU na Kazi za Meya/ Mwenyekiti wa Halmashauri
- Atakuwa ndiye Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Atakuwa na wajibu wa kuitisha na kuongoza mikutano yote ya Halmashauri ya kijiji, pamoja na Mikutano Mikuu ya Kijiji. Lakini endapo Mwenyekiti hayupo katika mkutano wowote, wajumbe wa mkutano unaohusika wanaweza kuchagua Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo;
- Atakuwa mwakilishi wa kijiji kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;
- Atawahudumia kwa usawa wanakijiji wote, bila kujali tofauti za Kisiasa, Kijinsia au za Kidini;
- Atakuwa mfano wa uongozi bora na utendaji bora wa kazi, kwa kuwa na shughuli zake mwenyewe za kujitegemea, ambazo zaweza kuigwa na wanakijiji wenzake.