KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

MAKONDA Atamani kuifuta Halmashauri ya Jiji la Arusha

Filed in Habari by on 31/05/2024 0 Comments

MAKONDA Atamani kuifuta Halmashauri ya Jiji la Arusha

MAKONDA Atamani kuifuta Halmashauri ya Jiji la Arusha

MAKONDA Atamani kuifuta Halmashauri ya Jiji la Arusha

MAKONDA Atamani kuifuta Halmashauri ya Jiji la Arusha,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshangazwa na Halmashauri ya Jiji kupatiwa Sh bilioni 7.7 na serikali Kuu na kutumia sh Milioni 500 na miradi ya maendeleo kukwama.

Makonda alipatiwa taarifa ya Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo waliwashangaa viongozi hao namna wanavyotekeleza majukumu yao na miradi kukwama licha ya kupewa fedha.

“Naibu meya nimejiuliza kwa nini tuna jiji kama miradi yote hiyo ilitakiwa kutekelezwa alafu haijatekelezwa tumebakiza mwezi mmoja na fedha zipo akili yangu ya haraka haraka ingekuwa ni mamlaka yangu ningewafukuza kazi wote,”amesema Makonda na kuongeza kuwa;

“Sio tu kuwafukuza kazi kule Marekani katiba inasema Rais anaweza kutoka madarakani kutokana na afya na mambo mengine hapa nawaza hakuna utaratibu unang’olewa kwenye majukumu yako kwa sababu umeshindwa kutimiza na kushtakiwa kupoteza muda wa wananchi,”

Alisema fedha iliyotumika kutoka serikali kuu ni asilimia 6.4 na miradi ya maendeleo haijatekelezwa licha ya fedha kuwa nazo.

“Ujue nawaza sijui watu wanapataje kazi najiuliza watu wanafanyaje mpaka wanaonekana wamaana jamani..kama ushirikina upo basi hii nchi inayo tukipita katika miradi tutaona hata jengo lao la utawala sijui linaendaje sijui ni kitu gani kinaendelea mmepewa kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo au ya kuonyesha nani mkubwa,” amesema Makonda.

Aidha Makonda amekemea tabia ya malumbano na kuvutana kwa watumishi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha suala ambalo limekuwa likisababisha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo licha ya serikali kutoa fedha.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *