RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili

Filed in Makala by on 24/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili

MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili,Maswali yanayoulizwa kwenye interview ya utendaji, Maswali ya usaili jkt, MASWALI ya interview TAKUKURU, Maswali ya interview ya uhasibu,Usaili wa kuandika, Maswali ya veta.

MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili

MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili,Maswali yanayoulizwa kwenye interview ya utendaji, Maswali ya usaili jkt, MASWALI ya interview TAKUKURU, Maswali ya interview ya uhasibu,Usaili wa kuandika, Maswali ya veta.

Kupata kazi ya ndoto zako si jambo jepesi, na inawezekana ikawa ni vigumu zaidi kama hujui waajiri wanataka nini kutoka kwako.

Ulimwengu wa ajira kwa kampuni kubwa ama ndogo unabadilika kwa kasi sana.

Lakini kuna eneo moja ambalo ni la muhimu kuzingatiwa kwa kila anayetafuta ajira.

USAILI WA ANA KWA ANA.

Mara nyingi inaaminika kuwa uwezo wako wa kujibu maswali mbele ya mtu ama jopo la watu linaweza kujenga ama kubomoa mustakabali wako wa kupata ajira.

Hivyo, unahitajika kujiandaa kikamilifu kabla ya kuingia kwenye chumba cha usaili wa ana kwa ana.

Yafuatayo ni mambo manane (8) muhimu yatakazokusaidia kufaualu usaili wakati wa kutafuta Kazi.

1.FANYA UTAFITI

  • Chunga usije kushtukizwa na maswali ndani ya chuma cha usaili, unaweza kupata tabu kuyajibu.
  • Kama kampuni au taasisi imekupatia majina ya watu watakaokusaili, jaribu kufanya utafiti wa kujua wao ni akina nani na wanafanya nini.
  • Pia itafiti kampuni ama taasisi hiyo kwa undani, Ipi ni biashara ama shughuli yao Kuu? Nani anaiongoza? Ina umuhimu ama nafasi gani katika fani husika? Na kampuni au taasisi zipi ni washindani wao wa Kibiashara.
  • Yawezekana ukawa unajiuliza utazipata wapi taarifa husika, sehemu nzuri ya kuanzia ni kwenye tovuti ya kampuni ama taasisi husika.
  • Chukua dondoo na andaa maswali ya kuuliza mwishoni mwa usaili ili kuwaonesha umefanya utafiti kiasi gani kuwahusu wao.
  • Utafiti ndiyo kazi ya muhimu ambayo unaweza kuifanya kabla kuingia kwenye chumba cha usaili, na hakika utaona faida yake.

2.FANYA MAJARIBIO

  • Baada ya utafiti wa kina andaa maswali ambayo unahisi utaulizwa na fanya majaribio ya kuyajibu.
  • Na endapo utakuwa na shida yeyote ile, rudi mtandaoni. Kuna tovuti kadha wa kadha ambazo hutoa maswali muhimu ambayo huulizwa kwenye chumba cha usaili kwa fani mbalimbali.
  • Uandaapo majibu yako, fikiria katika muundo wa kujieleza ulio na mtiririko bora. Andaa mifano hai ya namna gani umefanikisha ama unaweza fanikisha yale yote ambayo yanatakiwa katika nafasi ya ajira uliyoomba.
  • Hadithi fupi fupi za namna gani ulifaulu awali kwenye ajira zako nyingine na uzoefu wako inabidi zioneshe ni kwa namna gani utafaidisha kampuni inayokusaili endapo watakupa ajira.

3.VAA UVUTIE

  • Muonekano wa awali una nguvu kubwa sana. Baadhi ya waajiri hufanya maamuzi ndani ya sekunde 30 za mwanzo za kukutana na mtahiniwa wa usaili.
  • Unaweza ukawa na majibu mazuri ya maswali, lakini kama mavazi na haiba yako haikuwapendeza watahini wako, utakuwa unapigana katika pambano ambalo lazima ushindwe.
  • Virginia Eastman, ambaye ni mtaalamu mstaafu wa kutahini watu kwenye usaili anamuelezea bwana mmoja ambaye alimsaili kwa nafasi ya kuongoza kampuni ya habari.
  • “Harufu yake mbaya ilitangulia chumbani dakika tatu kabla yeye mwenyewe kuingia. Alikuwa amevaa hovyo: soksi zimechakaa, chakula kimenasia kwenye ukosi wa koti lake…yaani ilikuwa ni moja ya vitu vya ovyo kabisa ambavyo nimewahi kuvishuhudia.”
  • Bila kuuliza, bwana huyo aliikosa ajira aliyoomba.
  • Japo kampuni inaweza kuwa na sera ya mavazi ya kawaida, hawatakutegemea uende kwenye usaili ukiwa umevalia suaruali ya jeans. Wataalammu wa rasilimali watu wanashauri uvae suti.
  • Iwapo usaili si wa kazi rasmi, basi inashauriwa uvae shati jeupe na suruari au sketi.
  • Hakikisha muonekano wako ni nadhifu. Piga pasi siku moja kabla, na hakikisha hauli chakula cha michuzi au rangi rangi kabla ya kuingia kwenye usaili.

4.SALIMIA KWA KUJIAMINI

  • Hiki ni kitu ambacho wengi hukisahau lakini ni muhimu sana.
  • Mwajiri wako anaweza kukupunguzia alama kwa namna utakavyosalimia uingiapo chumba cha usaili.
  • Kama unasailiwa na mtu mmoja au zaidi unashauriwa uwape mkono huku ukiwaangalia machoni.
  • Salamu imara inaashiria kuwa unajiamini, unajua ukifanyacho na ni mweledi.
  • Lakini, chunga usijiamini kupitiliza, utaonekana kuwa ni mkorofi. Ila usipojiamini napo utaonekana kuwa ni muoga.
  • Pia hakikisha una kitambaa mfukoni, futa jasho kwenye viganja kabla ya kutoa salamu. Hakuna mtu anayependa kupewa mkono wenye jasho.
  • Na unapokuwa ndani ya chumba cha usaili hakikisha unawaangalia machoni , kuangalia chini ni dalili ya woga.

MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili

MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili,Maswali yanayoulizwa kwenye interview ya utendaji, Maswali ya usaili jkt, MASWALI ya interview TAKUKURU, Maswali ya interview ya uhasibu,Usaili wa kuandika, Maswali ya veta.

MAMBO 8 Muhimu ya Kukusaidia Kufaulu kwenye Usaili

5.TABASAMU!

  • Hili ni jambo jepesi kulitaja kuliko kulitenda hususani pale moyo wako unapokuwa unaenda puta, tumbo lako limevurugika na unaweza hata kusahau jina lako.
  • Hata hivyo, tabasamu ni lugha ya kimataifa ya kusema: “Nina furaha kuwa hapa, mimi ni mtu mwema.”
  • Hivyo basi tandaza tabasamu kubwa unapoingia kwenye chumba cha usaili. Usiliangushe tabasamu hilo wakati wote wa usaili. Ni njia bora ya kupata alama.
  • Hata hivyo, chunga mikao yako, usijilegeze kwenye kiti, kaa kikakamavu.

6.USIKUBALI WOGA UKAKUTAWALA

  • Ukiruhusu uoga ukutawale, kinachofuata kinaweza kuwa… balaa kubwa.
  • Uoga unaweza kufanya ukasahau kila kitu kwenye utafiti ulioufanya awali, unaweza ukafanya mikono yako ikawa inatetemeka na kutokwa na jasho.
  • Uoga pia unaweza ukakufanya kushindwa hata kutabasamu.
  • Kama unajua woga unaweza kukuathiri, basi jaribu kuvuta pumzi na kusema na moyo wako kuwa unaweza, na ndio maana umeitwa kwenye usaili.
  • Wataalamu wanasema kuwa, endapo utaweza kuushinda woga, basi yawezekana ukapata ujasiri wa hali ya juu na kufaulu usaili wako.

7.KUWA MCHANGAMFU

  • Kabla ya kuketi kwenye kiti cha usaili, tafakari “kipi kinakufanya uwe wa tofauti?”
  • Ukishajiuliza hivyo, usisite kuwa mchangamfu na kuonesha haiba yako, waoneshe kuwa wewe unastahili. Kumbuka si peke yako uliyeomba kazi hiyo na kuitwa kwenye usaili.
  • Usisahau pia kusema mambo mazuri kuhusu kazi uliyoiomba – na unapofikia mwisho wa usaili kumbuka kuisifia kampuni na vipi itakuwa fahari kwako kupata kazi hiyo.
  • Kumbuka uchangamfu na haiba yako ndiyo vitu pekee ambavyo vinaweza kukutofautisha na wengine.

8.USIKATE TAMAA NJIANI

  • Hata kama mambo yamekuwa mazito kiasi gani katika chumba cha usaili, usikate tamaa.
  • Kuna kipindi maswali yanakuwa magumu kiasi kwamba unaweza kudhani kuwa basi na kazi yenyewe ushaikosa.
  • Usifanye kosa la uamini kitu hicho, jitahidi, pambana mpaka dakika ya mwisho, yawezekana wewe ndiyo umefanya vizuri kuliko mtu yeyote katika usaili huo.
  • Pia yawezekana swali linalofuatia ndilo ambalo unalimudu kuliko yote yaliyopita.
  • Ni muhimu kujituliza kifikra mambo yanapokuwa magumu. Una nguvu kubwa ndani yako.

Fanyia kazi mambo haya manane utaona matokeo chanya!

Maswali ya interview ya kilimo, Maswali na majibu ya udereva, Maswali ya interview ya procurement,Maswali ya oral interview utumishi pdf, Maswali ya interview ya afisa maendeleo ya jamii.

Ajira Mpya Kila Siku pamoja na Kuitwa Kazini na kwenye Usaili Bofya Hapa

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , , , ,

Comments are closed.