Manara na Ali Kamwe nani Afisa Habari wa Yanga?
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Haji Sunday Manara na Ali Shabaan Kamwe nani Afisa Habari wa Yanga?
Ni swali ambalo liliibua mjadala katika mitandao ya kijamii kwamba kati ya Manara na Ali Kamwe nani ni Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Young Africans baada ya urejeo wa Haji Manara.
Hili ni swali ambao Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amelitolea majibu.
Aidha Ali Kamwe aliajiriwa kuwa Afisa Habari wa Young Africans baada ya Haji Manara kufungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili na Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF).
Hersi Said amesema kuwa, Ali Kamwe ataendelea na majukumu yake kama kuwa Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano huku wakiendelea kumtafutia nafasi Haji Manara.
“Klabu inamtambua Ally Kamwe kama Afisa Habari kwa sababu mpaka sasa mkataba wake unasema hivyo. Haji Manara alikuwa Afisa habari wetu na alifanya kazi nzuri sana katika muda wake na alipopata changamoto akafungiwa kama klabu tulihitaji mtu wa kuisemea klabu na hapo ndipo tulimchukua Kamwe”
“Kwa sasa Kamwe ndie Afisa Habari wetu na upande wa Manara yeye ni Mwanachama wetu na tunaangalia ni sehemu gani ambayo tutamuweka kwenye klabu,” alisema Hersi katika kipindi cha Jana na Leo Cha radio ya Wasafi FM
Hivi karibuni Kamwe alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Young Africans baada ya mkataba wa awali kufikia tamati.
Pia Haji Manara naye alisaini mkataba wa mwaka mmoja na kumfanya awe na mkataba wa miaka miwili ambao utamalizika mwaka 2026.
Soma na hizi: Yanga vs Vital’O FC Kupigwa Azam Complex