MAPYA Yaibuka Usajili wa Lameck Lawi Simba
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MAPYA Yaibuka Usajili wa Lameck Lawi Simba
MAPYA Yaibuka Usajili wa Lameck Lawi Simba, baada ya Simba kumtambulisha beki wa kati wa Coastal Union, Lameck Lawi baada ya kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu, mapya yameibuka.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Coastal kimeliambia Gazeti la Mwanaspoti kuwa, Lawi sio mchezaji wa Simba kama ilivyomtangaza huku kikiweka wazi Wekundu wa Msimbazi hao wamemkosa staa huyo kutokana na kuchelewesha malipo.
“Simba ni kweli walikuja mezani kufanya mazungumzo ya kumsainisha Lawi na makubaliano yalienda vizuri kwa kukubaliana timu hiyo kulipa fedha za usajili muda ambao tulikubaliana, lakini hawakufanya hivyo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;
“Tumerudisha fedha ya Simba ambayo imeingia tofauti na makubaliano tunashangazwa na timu hiyo kuamua kutangaza mchezaji wetu kuwa ni wao hili sio sawa.”
Beki huyo ameisaidia Coastal Union FC kuwa katika nafasi ya nne ya Msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 25 na kufanikiwa kukusanya pointi 34 na kukata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2024/2025.