Mashindano ya UMITASHUMTA 2024 Mikoa Yaanza
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Mashindano ya UMITASHUMTA 2024 Mikoa Yaanza
Mashindano ya UMITASHUMTA 2024 Mikoa Yaanza, Timu za riadha kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania, zimeanza kushindana katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ambayo yameingia siku ya nne Mkoani Tabora.
Hatua ya awali ya Mchezo wa riadha umeanza asubuhi ya leo (jana) tarehe 09 Juni 2024 katika mzunguko wa uwanja B uliopo shule ya Sekondari Tabora Wavulana, ikihusisha wasichana, wavulana kawaida na maalum kwenye mbio za umbali tofauti.
Michezo ya leo pia imehusisha kutupa Tufe wasichana na wavula kawaida pamoja na maalum, huku upinzani mkali ukionekana katika mashindano ya mwaka huu kutokana na maandalizi mazuri yanayochangiwa na maboresho ya miundombinu.
Mratibu wa Mchezo wa riadha katika Mashindano ya UMITASHUMTA 2024 Neema Chongolo, amesema kuwa kumekuwa na mwanzo mzuri na kunatarajiwa ushindani mkubwa kutokana na mikoa inayoshiriki kuonekana kujiandaa vizuri.
“Kila mwaka kunakuwa na mabadiliko hususan kwenye maandalizi, mwaka huu unaonekana hamasa imekuwa kubwa lakini pia wanamichezo wanaonesha wameandaliwa vizuri na sisi kwa upande wa uratibu tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda vizuri” amesema Neema.
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISETA 2024 yananaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, yakiwa na kauli Mbiu isemayo “Tunajivunia mafanikio katika sekta ya elimu, michezo na Sanaa, Hima Mtanzania shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024”