MASWALI ya Interview Ajira za Watendaji wa Vijiji
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MASWALI ya Interview Ajira za Watendaji wa Vijiji
MASWALI ya Interview Ajira za Watendaji wa Vijiji,Maswali ya interview UTUMISHI, MASWALI ya interview NA MAJIBU yake, Maswali ya interview bot,Maswali ya usaili wa polisi,Maswali ya usaili wa kuandika, Maswali ya oral interview UTUMISHI, Maswali ya usaili Mtendaji wa kijiji, Interview Questions.
Mahojiano kimsingi ni mazungumzo yaliyopangwa ambapo mshiriki mmoja anauliza maswali, na mwingine hutoa majibu. Katika lugha ya kawaida, neno “mahojiano” linamaanisha mazungumzo ya moja kwa moja kati ya mhojiwa na mhojiwa. Ulifanya kazi kwa bidii kwenye wasifu wako na ombi la kazi, na sasa umeitwa kwa mahojiano ya kazi ya kibinafsi.
Uko hatua moja karibu na kazi yako ya ndoto. Ni wakati wa kuelewa jinsi ya kufanikiwa katika mahojiano ya kazi, ili uweze kupata kazi. Hapa kuna mambo muhimu zaidi ambayo unapaswa kukumbuka.
1.Vaa ipasavyo, Panga vazi linalolingana na utamaduni wa kampuni unayotuma ombi. Ikiwa kampuni haina kanuni ya mavazi, ni wazo zuri kuvaa kibiashara ya kawaida. Acha kaptula yako na tank top nyumbani, na kuvaa shati na jozi ya suruali ndefu. Daima ni bora kuvikwa zaidi kuliko chini. Jaribu vazi lako kabla ya mahojiano ili kuhakikisha kwamba linalingana na linaonekana nadhifu.
2.Fika kwa wakati, Usiwahi kufika kwenye usaili wa kazi kwa kuchelewa! Ni bora kufika dakika 15 kabla ya muda uliopangwa ikiwa utalazimika kujaza karatasi. Hii pia hukuruhusu kutulia na kuangalia mienendo ya ofisi. Ikiwa hujui eneo ambalo kampuni iko, fanya mtihani wiki moja au mbili kabla ili kuhakikisha kuwa hutapotea..Ikiwa unaendesha gari, andika mahali unapoweza kuegesha gari lako.
3.Zingatia tabia, yako Kuwa na adabu na msalimie kila mtu unayekutana naye, hata watu unaokutana nao kwenye lifti. Unapoingia kwenye mahojiano, mpe anayehoji salamu. Sekunde hizi chache za kwanza zinaweza kufanya au kuvunja mahojiano yako. Mwishoni mwa mahojiano, usisahau kumshukuru anayekuhoji kwa kukupa fursa ya mkutano. Unapotoka kwenye kampuni, sema kwaheri kwa mpokeaji.
4.Zingatia lugha ya mwili wako, Lugha mbaya ya mwili, kama vile kucheza na kalamu, kutafuna sandarusi, kuteleza, na hata kunyoa nywele za nyuma, inaweza kuwa kikengeusha fikira. Ukiona una tabia ya kufanya mojawapo ya haya, jizoeze kuepuka tabia hizi mbaya. Unaweza kuzibadilisha kwa kutumia lugha chanya ya mwili ambayo ni pamoja na kutikisa kichwa, kugusa macho, kutabasamu na mkao thabiti.
5.Uliza maswali ya utambuzi, Wasailiwa wengi humaliza mahojiano kwa kuruhusu mtahiniwa kuuliza maswali. Bila kujali jinsi unavyojua kampuni vizuri na jinsi mhojiwa anakuambia juu ya kazi, lazima uulize maswali machache. Kadiri maswali yako yanavyokuwa na ufahamu zaidi, ndivyo utakavyomvutia anayekuhoji.
Download wimbo mpya wa Diamond
MASWALI YA USAILI AJIRA ZA WATENDAJI WA VIJIJI
MASWALI NA MAJIBU YA SAILI MBALIMBALI ZILIZOFANYIKA MAENEO YA HALIMASHAURI, MANISIPAA PAMOJA NA MAJIJI MBALIMBALI NCHINI TANZANIA KATIKA NAFASI YA KAZI YA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA TATU.
QN1.Kila Afisa mtendaji wa kijiji anatakiwa kutunza daftari la mali za kudumu, Daftari hilo litaonyesha mambo gani? yaeleze kwa upana.
a) Aina ya mali ya kudumu, hati na mahali ilipo.
b) Jina la mmiliki.
c) Gharama ya mali ya kudumu.
d) Tarehe ya kununulia mali ya kudumu. e) Ongezeko la thamani ya mali ya kudumu.
f) Mauzo na taarifa nyingine kuhusu mali ya kudumu.
g) Kila aina ya mali iliyoandikwa kwenye ukurasa wa peke yake
QN2.Mambo gani ya kuzingatia katika tahadhari ya majanga? yaelezee.
a) Hatua ya kwanza kubuni taratibu, mbinu na mikakati ya kuzuia majanga ili yasitokee au kupunguza athari zake pindi yanapotokea.
b) Hatua ya pili kuwezesha jamii kufuata taratibu zote za kutekeleza mbinu na mikakati ili kujenga uwezo kwa jamii kudhibiti majanga yasitokee.
QN3.Eleza njia kuu za kudhibiti mapigano katika jamii?
a) Kuimarisha utawala bora katika ngazi zote za halimashauri yaani ngazi za mitaa,vijiji na kata.
b) Kuhamasisha uelewa kuhusu misingi ya utawala bora katika ngazi zote.
Kujenga umoja wa kuheshimiana na kushirikiana katika makundi mbalimbali katika jamii moja.
d) Kujenga umoja wa kuheshimiana na ushirikiano kati ya uongozi na jamii za kijiji au kata au majirani.
QN4.Ni mambo gani ya kuzingatia ili kikao kiwe halali?
a) Mahudhurio
b) Mwenyekiti.
c) Katibu.
d) Idadi ya wajumbe. e) Agenda.
f) Muhtasari.
QN5.Afisa mtendaji wa kijiji kama mtendaji mkuu wa shughuli zote katika eneo lake na pia kama mlinzi wa amani,unalo jukumu kubwa la kuhakikisha migogoro yote inayojitokeza inashughulikiwa na kupewa ufumbuzi wa kudumu.
Katika uendeshaji wa shughuli za serikali, uzoefu unaonyesha kuwa katika maeneo mengi hususani kwenye ngazi ya kijiji kuna aina mbalimbali za migogoro.
Eleza aina tano za migogoro iliyopo katika ngazi za kijiji utakayotakiwa kushughulika nayo?
a) Migogoro kati ya koo na koo. b) Migogoro kati ya kaya na kaya.
c) Migogoro kati ya wananchi na wawekezaji.
d) Migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
e) Migogoro kati ya serikali ya kijiji na taasisi za mikopo.
QN6. Utahakikisha vipi taarifa za makusanyo ya fedha yakiwemo ya ushuru,ada na mapato mengine yanakusanywa ndani ya kijiji kwa mujibu wa sheria?
a) Daftari la malipo.
b) Stakabadhi za malipo.
c) Risti mbalimbali.
d) Nyaraka za malipo.
QN7.Eleza jinsi utakavyosimamia matumizi bora ya rasilimali za umma katika kijiji chako.
a) Kupanga.
b) Kuweka wasimamizi.
c) Kuunda vikundi.
d) Njia za udhibiti.
e) Mbinu za mawasiliano.
QN8. Kitovu cha vita ya umaskini ni kaya .Umaskini na hali duni ya maisha vitaweza kumalizika tu iwapo wananchi wenyewe wataamua kuondokana na hali hiyo kwa kutumia nguvu-kazi iliyopo, rasilimali zilizopo kwenye maeneo yao na misaada kutoka serikalini na sehemu nyingine ikiwemo ya wadau wa maendeleo pale hali inaporuhusu.Ili kupunguza na kuondokana na umasikini, Maafisa watendaji wa vijiji au mitaa kwa kushirikiana na viongozi na wataalam wengine, wanatakiwa kuchukua hatua mbalimbali,eleza hatua tano(5) utakazochukua kukabiliana na hali hiyo?
a) Kuelewa hali ya umaskini katika maeneo yao.
b) Kuainisha sababu za umaskini kwa kushirikiana na wananchi.
c) Kuelekeza kila mwananchi aelewe tatizo la umaskini na ajenge azma ya kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini.
d) Kuwaeleza wananchi kutumia fursa zilizopo ili kuondokana na hali hiyo. e) Kuunda vikundi vitakavyosaidia kuepukana na hali ya umaskini.
QN9.Moja kati ya majukumu na kazi za kamati za halmashauri ya kijiji ni kuhakikisha kuwa kanuni za kilimo bora na malengo ya kilimo, ufugaji bora na uvuvi bora zinafuatwa na kutekelezwa.
Taja namna utakavyotekeleza?
a) Kutayarisha mashamba mapema,
b) Kusafisha mashamba baada ya mavuno.
c) Kupanda mapema kwa kufuata mazingira ya hali ya hewa.
d) Kuhifadhi mazao gharani.
e) Kuchagua mbegu bora na kuweka mbolea mashambani.
QN10.(a) Taja mambo makubwa ya kimuungano ambayo Tanzania bara na visiwani wanashirikiana.
- Katiba ya jamhuri na serikali ya Jamhuri ya Muungano.
- Mambo ya Nchi za Nje.
- Ulinzi na Usalama.
- Polisi.
- Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
- Uraia.
- Uhamiaji.
- Mikopo na biashara ya Nchi za Nje.
- Utumishi katika serikali ya Jamuhuri ya Muungano.
- Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania.
- Bandari,mambo yanayohusika na usafiri wa anga,posta na simu
Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti);mabenki(pamoja mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;fedha za kigeni. - Leseni ya viwanda na takwimu.
Elimu ya juu. - Maliasili ya mafuta,pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa,na gesi asilia.
- Baraza la taifa la mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
- Usafiri na usafirishaji wa anga.
Utafiti. - Utafiti wa hali ya hewa.
Takwimu. - Mahakama ya Rufani ya Jamuhuri ya Muungano.
- Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo.
(b) Taja viashiria vitano vya umaskini hapa Tanzania.
- Kutokujua kusoma na kuandika.
Kutokuwa na uhakika wa kupata chakula,mavazi na malazi. - Uhaba wa maji safi na salama.
- Huduma duni za afya.
- Vifo vingi vya wananchi.
- Muda mfupi wa maisha.
- Utapiamlo kwa watoto na watu wazima.
- Uchakavu wa mazingira.
- Ukosefu wa ajira na kipato duni.
- Kutokufahamu masuala muhimu ya jamii.
QN11.Ukiwa kama mtendaji wa kijiji utakutana na majalada, nyaraka mbalimbali za serikali na vitu vingine vingi katika kazi zako za kila siku.
Je ni mambo gani muhimu ya kuzingatia unapokutana na nyaraka hizo?
a) Kuhakiki hizo nyaraka.
b) Kuzichambua hizo nyaraka.
c) Kuzipanga na kuzitofautisha
d) Kuzihifadhi/kuzitunza kwa kila nyaraka katika majalada(file) lake katika
masijara.
QN12.Taja majukumu ya mkutano mkuu wa kijiji.
a) Kupokea na kujadili taarifa za utekelezajiwa shughuli mbalimbali.
b) Kupokea na kujadili mapato na matumizi ya fedha.
c) Kupokea na kujadili taarifa za makusanyo ya fedha yakiwamo ya ushuru,ada na mapato mengine yanayopaswa kukusanywa ndani ya kijiji kwa mujibu wa sheria.
d) Kupokea na kujadili taarifa za watu walioomba kupewa ardhi.
e) Kupokea na kujadili mapendekezo yaliyotolewa na halmashauri ya kijiji au kitongoji.
f) Kufanya maamuzi yanayozingatia demokrasia.
g) Kuchagua mwenyekiti na wajumbe wa halmashauri ya kijiji.
h) Kujadili na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo.
i) Kuidhinisha utungwaji wa sheria ndogo kabla ya kupelekwa kwenye halmashauri wilaya kwa ajili ya kupitishwa kwa manufaa ya kijij.
QN13. Taja misingi ya utwala bora.
a) Utawala wa sheria.
b) Demokrasia.
c) Ushirikishwaji.
d) Uwazi.
e) Uwajikibikaji.
Ufanisi.
QN14. Taja vyanzo vitano vya mapato halmashauri za wilaya?
a) Mapato ya ndani.
b) Wahsani/wafadhili.
c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha kama vile banki n.k d) Michango ya jamii.
e) Ruzuku kutoka serikali kuu.
QN15. Taja alama muhimu za taifa?
a) Mwenge wa uhuru.
b) Wimbo wa taifa.
c) Bendera ya taifa.
d) Fedha ya taifa.
e) Nembo ya taifa.
QN16. Taja maadili matano(5) ya utumishi wa umma?
a) Kufanya kazi kwa bidii.
b) Kutoa huduma bila upendeleo.
c) Utii kwa serikali.
d) Kutokupokea rushwa.
e) Kutunza siri za serikali.
f) Kutoa huduma bora.
g) Kufanya kazi kwa uadilifu.
h) Uwajibikaji kwa umma.
i) Kuheshimu sheria.
j) Matumizi sahihi ya taarifa
QN17. Taja rangi za bendera ya Tanzania na maana zake.
a) Nyeusi-Inawakilisha watu wa Africa.
b) Njano-Inawakilisha madini.
c) Kijani-Inawakilisha mimea.
d) Bluu-Inawakilisha mito,maziwa na bahari.
QN18. Taja majukumu ya Afisa mtendaji wa kijiji.
a) Atakuwa mtendaji na mshauri mkuu wa serikali ya kijiji na kamati zake katika mipango ya maendeleo ya jamii na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
b) Atakuwa Afisa mhasibu wa serikali ya kijiji na atasimamia mapato na matumizi yz serikali.
c) Atakuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
d) Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji.
e) Atakuwa katibu wa kamati ya halmashauri ya kijiji.
f) Atatafsiri sera,ataratibu na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogodondogo. g) Atawajibika kwa mtendaji wa kata.
h) Atakuwa kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalamu katika kijiji.
i) Atasimamia matumizi bora ya nguvu kazi.
j) Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa,umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
k) Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi,wataalamu mbalimbali na NGOs waliopo katika kijiji.
QN19.In state set up! What does separation of power mean?
Separation of power-Refers to the states being separated and vested in the three organs/branches of the states.
These branches are The Legislature, The judiciary and The executive
Functions of each organ
- a) The legislature
To make and amends laws. - To discuss and pass the budget.
- To question ministers during parliamentary season.
b) The judiciary
- To interpreters laws.
- To provide rights for injury or harm person.
c) The executive
To enforce laws and to ensure every one obey the laws.
QN20. (a) Village governments have been given mandate to make by-laws; Which institution has delegated this function?
-The institution delegated this function is the legislature
(b) What is good governance?
-Is a way of measuring how public institutions conduct public affairs
and manage public
resources in a preferred way.
(c) Mention any five pillars of good governance?
- Rule of law.
Democracy. - Participatory.
- Transparency.
- Accountable.
- Responsiveness. Consensus oriented.
- Effective and efficiency.
QN21. LGAs have various sources of revenue. Can you mention at least 3 sources of revenue for the following categories of LGAs.
include
(a) District councils?
(b) Urban councils?
(c) Village government?
-There are five main sources of revenue in District & urban councils these
Own source. Donors.
- Community contributions.
Intergovernmental transfer.
-Sources of revenue in village government - Percent of the unit or field sales/mauziano ya kiwanja au shamba kuna asilimia(10%) kijiji huwa kinachukua.
- Any others sources of revenue passed by village assembly.
QN22. Mention any five roles of local government to the community development?
a) To formulate, coordinate and supervise the implementation of all plans for the economic, commercial, industrial and social development in its area of jurisdiction.
b) To ensure the collection and proper utilizations of the revenues.
c) To
regulate and monitor the collection and utilization of revenue of village councils and township authorities.
d) Take all necessary measures for the prevention of soil erosion and the protection of crops.
e) To prepare, undertake, regulate and control schemes for improved housing layout and settlement.
f) To provide services for the improvement of livestock.
QN23.Nini maana ya Afisa mtendaji?
-Ni mtu mwenye utaalamu katika eneo au taasisi, ambapo kazi yake ni kufuatilia namna taasisi zinavyofanya/kutenda kazi mara nyingi mtendaji ni mtu wa kuajiriwa tofauti na viongozi wanaochaguliwa na wananchi.
QN24. Define the following terms.
- Local government Authority. Is a type/kind of government vested power to perform functions within the specified areas.
- Examples of local government authorities
a) Rural authorities District councils, Township Authorities and village councils
b) Urban Authorities; City council, Municipal and Town council By-laws. Is a rule or law established by an organization to regulate it self as allowed or provide for by some higher authority OR By-law can be defined as a law of local or limited application passed under authority or higher law stating things they may regulate.
Rule of law. Is a situation in which the laws of country are obeyed by
everyone.
QN25.(a) How many types of councilors do we have in council.
councilors
According to the book of ” MJUE DIWANI❞ there are four(4) types of
Elected councilors.
Appointed councilors.
• Such number of women members who are qualified to be elected to the council.
Member of parliament representing constituencies.
(b) How councilors elected?
According to the book of “mjue diwani” how councilors elected?
⚫ Elected during general election which held for every five years.
• Elected during by election when a member dies, resigns,his election voided by court, member ceased to be a member of political party sponsored him.
• Such number of women members who are qualified to be elected to the council.
QN26. (a) Bunge ni nini? Ni chombo cha kutunga sheria ambacho kimepewa mamlaka kwa mjibu wa katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 4,61,64.
(b) Kuna aina mbili za bunge zitaje?
Bunge la chumba kimoja ambako wawakilishi wote wa wananchi hukaa pamoja na kufanya maazimio pamoja.
Bunge la vyumba viwili ambako kitengo kikubwa kina kazi ya kutunga
sheria na wabunge huchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika majimbo ya uchaguzi.
QN27. Ni faida zipi zinazoweza kudumisha utamaduni bora wa Taifa letu? Taja angalau tano.
a) Kutambua na kulinda rasilimali, mazingira na urithi wa utamaduni.
b) Kuhakikisha na kuhimiza usawa katika matumizi bora na mgawanyo wa haki na rasilimali.
c) Utamaduni husaidia kuenzi na kutunza tabia njema na kukemea vitendo viovu kama vile matumizi ya madawa ya kulevya,ubakaji,unyanyasaji n.k
d) Utamaduni husaidia kutambua na kuhimiza kazi halali kuwa ni msingi wa maisha na maendeleo ya binadamu.
e) Kuhimiza utunzaji wa rasilimali za Taifa.
f) Kupiga vita udhalilishaji wa kijinsia.
g) Kuhimiza tabia ya kuheshimu utu,watu na sheria kwa manufaa ya maendeleo.
h) Kujenga tabia ya usafi,uhifadhi na matumizi bora ya rasilimali na mazingira.
i) Utamaduni husaidia kuhimiza na kujenga Taifa lenye nidhamu.
j) Kujenga taifa na kutambua,kuenzi na kuheshimu vitambulisho vya Taifa.
QN28. Tanzania iliamua rasmi kuingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi mnamo mwaka 1992. Lengo la mfumo huu ni kuleta ushindani na ufanisi katika kuwahudumia wananchi na kupanua wigo wa kwa ujumla na si
uwazi,ukweli,uwajibikaji,na
utawala bora
vinginevyo.
Miongoni mwa taratibu zinazopaswa kufuatwa katika kujenga demokrasia ya kweli ni pamoja na watu kujijengea utamaduni Eleza tamaduni hizo.
a) Uvumilivu na staha kwa mitazamo na maoni tofauti ya kisiasa.
b) Kufuata na kuheshimu mawazo ya walio wengi na pia kusikiliza na kukubali mawazo ya wachache iwapo yana manufaa na umuhimu mkubwa kwa kitongiji au mtaa, kijiji, kata, wilaya, mkoa au Taifa kwa ujumla.
c) Kutumia nguvu ya hoja na siyo hoja za nguvu.
d) Kupingana bila kupigana.
e) Kujikosoa na kukosoana bila kuleana.
QN29.Taja majukumu ya kamati ya fedha, uchumi na mipango.
a) Kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kijijini.
b) Kuweka hesabu sahihi za shughuli zote kijijini.
c) Kupendekeza matumizi bora ya ardhi ya kijiji kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kilimo,ufugaji na ujenzi.
d) Kusimamia ukusanyaji wa kodi na ushuru uliowekwa na Halmashauri ya wilaya na Serikali ya kijiji.
e) Kutafuta njia mbalimbali za kuongeza mapato kijijijini.
f) Kuhakikisha kanuni bora za kilimo na malengo ya kilimo,ufugaji na uvuvi bora zinafuatwa na kuendelezwa.
QN30. Taja mbinu za kutatua migogoro katika jamii.
a) Kutawala maamuzi.
b) Mbinu shirikishi.
c) Kuepuka suluhu ya mgogoro.
d) Kuepusha shari.
e) Kukubaliana.
QN31.Maafisa watendaji wa kijij wamepewa uwezo wa kukamata au kuagiza kukamata kutokana na sheria zipi? Zitaje.
a) Sheria ya serikali za mitaa(mamlaka za wilaya) Namba 7 ya mwaka 1982.
b) Sheria ya serikali za mitaa(mamlaka za miji) Namba 8 ya mwaka 1982.
c) Sheria ya mwenendo wa kesi za jinai Namba 9 ya mwaka 1985.
d) Sheria ya mahakama za mahakimu Namba 2 ya mwaka 1984.
QN32.Taja sababu ambazo zinasababisha serikali kusisitiza maendeleo vijijini?
a) Kijijini ndipo mahali shughuli za kilimo zinapofanyika ambapo kilimo ni utii wa mgongo wa Taifa.
b) Miundo mingi vijijini haipatikani mfano barabara,huduma za afya n.k
c) Uelewa mdogo miongoni mwa wananchi hasa wanaoishi vijijini.
d) Kipato duni miongoni mwa wananchi wanaoishi vijijini na wengine kushindwa kumudu mahitaji muhimu.
QN33. Taja msingi ya kidemokrasia.
a) Ushirikishwaji wa wananchi.
b) Kujikomboa.
c) Madaraka kwa umma.
d) Uchaguzi huru na haki.
e) Uhuru wa binafsi.
f) Haki za binadamu na wajibu (sura ya kwanza sehemu ya tatu (12-25) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977)
g) Mgawanyo wa madaraka na vyombo vikuu vya uongozi wan chi ambavyo ni bunge,serikali na mahakama.
QN34. Taja walinzi wa amani.
a) Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya,miji,manisipaa au jiji.
b) Afisa Tarafa.
c) M aafisa watendaji wa vijiji au mitaa.
QN35.Eleza nafasi ya Afisa mtendaji wa mtaa katika utekelezaji wa ulinzi shirikishi?
a) Kushawishi wananchi katika kijiji/mtaa kuanzisha mtandao wa ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji na mtaa.
b) Kuratibu shughulu zote za mtandao wa ulinzi shirikishi.
c) Kuitisha mikutano ya ujirani mwema,kutangaza mpango wa ulinzi shirikishi kwa nguvu zote ili kila mwananchi aone umuhimu wa kushiriki katika na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kujua maeneo yenye udhaifu ambayo yanaweza kutumiwa na wahalifu.
d) Kushirikiana na jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola sambamba na askari wa Halmashauri katika utekelezaji wa mikakati ya kuzuia uhalifu na vurugu kwa kuihusisha jamii.
ndugu zangu ikumbukwe kwamba haya ni mawazo ya wadau pamoja na group letu la questions for interviwes kilichofanyika ni kuunganisha mawazo hayo, maswali mengine bado hayajapatiwa majibu yakiwa tayari tutatuma.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Interview Questions, interview za watendaji wa vijiji, Maswali na majibu usaili wa Afisa Watendaji wa Vijiji., MASWALI ya Interview Ajira za Watendaji wa Vijiji, Maswali ya interview bot, Maswali ya Interview katika Ajira za Watendaji wa Vijiji, MASWALI ya interview NA MAJIBU yake, Maswali ya interview UTUMISHI, Maswali ya oral interview UTUMISHI, Maswali ya usaili, Maswali ya usaili Mtendaji wa kijiji, Maswali ya usaili wa kuandika, Maswali ya usaili wa polisi, Maswali ya usaili/Interview kwa utendeji wa mtaa katika halmashauri mbalimbali, Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi