RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MASWALI Yanayoulizwa Mara kwa Mara Bodi ya Uhasibu

Filed in Makala by on 27/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

MASWALI Yanayoulizwa Mara kwa Mara Bodi ya Uhasibu

MASWALI Yanayoulizwa Mara kwa Mara Bodi ya Uhasibu

MASWALI Yanayoulizwa Mara kwa Mara Bodi ya Uhasibu

MASWALI Yanayoulizwa Mara kwa Mara Bodi ya Uhasibu,Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara NBAA,Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ni Taasisi inayosajili na kusimamia Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu na kudhibiti taaluma ya Uhasibu nchini.

NBAA Ilianzishwa kwa sheria ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu sura ya 286 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ipo chini ya Wizara yenye dhamana ya fedha.

Bodi hiyo ilianzishwa mwaka 1972 na kuanza kufanya kazi zake rasmi kuanzia tarehe 15 Januari 1973.

Tangu kuanzishwa kwake, NBAA imetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taaluma ya uhasibu nchini Tanzania hasusani katika kuhamasisha, kusajili, kuwekaji viwango na usimamizi wa mitihani.

NBAA inajitahidi kutoa mchango mkubwa katika kuhamasisha utawala bora kupitia uendelezaji wa taaluma ya uhasibu nchini Tanzania.

Taaluma ya uhasibu ina mchango muhimu katika kuchochea kujiamini kibiashara na kusaidia ukuaji wa kiuchumi.

Wanachama wa NBAA wanatoa mchango mkubwa wa kushawishi sekta ya umma na binafsi kama chombo cha kitaalamu.

NBAA pia inasaidia wanachama na wadau kwa njia ya huduma mbalimbali na kutoa sauti ya pamoja kwa taaluma.

Katika Makala hii utapata kufahamu Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Bodi ya Uhasibu (NBAA) na Majibu yake.

Swali: Je nikiwa sina masomo matatu niliyofaulu vizuri (credit) katika elimu ya Sekondari, lakini napenda kujiunga katika fani ya uhasibu, nifanye nini?

Jibu: Kuna vyeti vingine vinavyotambuliwa na NBAA: kama cheti cha NABE hatua ya II na kufaulu masomo yasiyopungua manne uliyofaulu vizuri (passes grade) pamoja na cheti cha kidato cha nne(IV).

AU Barua ya Matokeo ya Hatua ya Msingi ikionyesha kuwa umefaulu mtihani huo ambao unaendeshwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.

Zaidi ya hayo ni lazima uwe umemaliza Elimu ya Sekondari ikionyesha masomo uliyofanya na kufaulu.

Swali: Masharti ya kujiunga kufanya mitihani ya ATEC I ni yapi?

Jibu: Masharti ya kujiunga katika mitihani ya ATEC ni kuwa na cheti cha kumaliza Elimu ya Sekondari na kufaulu vizuri (credit) masomo yasiyopungua matatu (3) na kufaulu (pass grade) masomo mawili (2) ikiwemo Kiingereza na Hisabati.

AU cheti cha kumaliza Elimu ya Sekondari kidato cha sita (VI) na kufaulu Masomo Makuu mawili au moja na somo la ziada, alimradi uwe umefaulu Hisabati katika Elimu ya Sekondari ya Kidato cha nne (IV) angalau kwa alama ya D.

AU Cheti cha mwaka mmoja kutoka chuo kinachotambulika pamoja na ufaulu wa alama ya D au zaidi katika masomo ya Kiingereza na Hisabati katika cheti cha kidato cha nne

AU Vyeti vingine ambavyo vitakavyoendelea kutambuliwa na Bodi wakati kwa wakati.

Swali: Ni mitihani gani inayoendeshwa na NBAA?

Jibu: NBAA inaendesha mitihani katika ngazi mbili za kitaaluma; Mitihani kwaajili ya Cheti cha Uandishi na Utunzaji Vitabu vya Hesabu Ngazi ya I & II (Accounting Technician Examinations – ATEC Level I & II) yenye masomo manne manne kila ngazi na Mitihani ya Kitaaluma ya Uhasibu – Professional Examinations ambapo mhitimu hupata shahada ya Uhasibu yaani Certified Public Accountant (CPA).

Mitihani ya ATEC iko katika ngazi mbili ; ATEC 1 na ATEC II, Mitihani ya CPA iko katika hatua tatu ; Ngazi ya Msingi yenye masomo matano, Ngazi ya Kati yenye masomo sita na Ngazi ya Mwisho yenye masomo manne.

Swali: Nimemaliza Elimu ya Sekondari hivi karibuni. Je, ni kozi zipi ninazoweza kuchukua?

Jibu: NBAA ni Taasisi ya kutahini na huwa hakiendeshi kozi zozote za uhasibu bali hushirikiana na vyuo vinavyoendesha masomo ya uhasibu ambavyo inavitambua ili viendeshe mafunzo hayo kwa wanafunzi wanaojiandaa kwa mitihani ya Bodi.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.