MATOKEO Simba Queens vs FAD Djibouti August 19-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Klabu ya Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya FAD Djibouti katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki uliopigwa katika Uwanja wa Abebe Bikila.
Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Mshambuliaji Asha Rashid ‘Mwalala’ aliyefunga mabao matatu ‘hat trick’ pamoja na Jentrix Shikangwa aliyefunga bao la kwanza dakika ya 24.
Bao jingine limefungwa na Elizabeth Wambui aliyefunga bao la pili Katika dakika ya 30, huku Asha Rashid ‘Mwalala’ akifunga bao la tatu dakika ya 73, bao la nne dakika 80 na kufunga bao la tano na la mwisho dakika ya 90.