RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MATOKEO ya Uchaguzi Jimbo la Kwahani Zanzibar June 08-2024

Filed in Habari by on 09/06/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

MATOKEO ya Uchaguzi Jimbo la Kwahani Zanzibar June 08-2024

MATOKEO ya Uchaguzi Jimbo la Kwahani Zanzibar June 08-2024, Matokeo ya Ubunge Jimbo la Kwahani Zanzibar 2024, Pele ashinda Ubunge Jimbo la Kwahani Zanzibar, Pele ashinda Ubunge kwa Kura 7092 halali.

MATOKEO ya Uchaguzi Jimbo la Kwahani Zanzibar June 08-2024

MATOKEO ya Uchaguzi Jimbo la Kwahani Zanzibar June 08-2024, Matokeo ya Ubunge Jimbo la Kwahani Zanzibar 2024, Pele ashinda Ubunge Jimbo la Kwahani Zanzibar, Pele ashinda Ubunge kwa Kura 7092 halali.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani jijini Zanzibar, Bi. Safia Iddi Muhammad imemtangaza Bw.Khamis Yussuf Mussa (Pele) kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akinyanyua juu hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi. (Picha na INEC).

Mussa maarufu Pele ameibuka mshindi wa kiti hicho baada ya kupata kura 7,092 kati ya kura halali 7,383 zilizopigwa na kuwabwaga wagombea wenzake 13 waliokuwa wakichuana katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika leo tarehe 8 June 2024.

Jimbo la Kwahani lilikuwa na wapiga kura 11,936 na waliojitokeza kupiga kura ni 7,522 ambapo kura 139 zilikataliwa hivyo kufanya kura halali zilizopigwa kuwa ni 7,383.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad akimkabidhi hati ya ushindi Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumtangaza kuwa ndiye mshindi wa Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani. (Picha na INEC).

Vyama 14 vilisimamisha wagombea katika Uchaguzi huo mdogo wa kiti cha Ubunge jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Wagombea wengine na kura walizopata katika mabano ni pamoja na Bi. Jarade Ased Khamis wa AAFP (06), Bi. Madina Mwalim Hamad wa ADA TADEA (49), Bi. Shara Amran Khamis wa ADC (83), Bi. Zainab Maulid Abdallah wa CCK (21), Bw. Abdi Khamis Ramadhan wa CUF(79), Bw. Bashir Yatabu Said wa Demokrasia Makaini (14), Bi. Nuru Abdulla Shamte wa DP(07) na Bw. Kombo Ali Juma wa NRA (05)

Wengine ni Bi. Mwanakombo Hamad Hassan wa NLD (08), Bw. Amour Haji Ali wa SAU(07), Bi. Naima Salum Hamad wa UDP(01), Bi. Mashavu Alawi Haji wa UMD (05) na Bi. Tatu Omary Mungi wa UPDP(06).

Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akionesha hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi. (Picha na INEC).

Uchaguzi katika Jimbo la Kwahani umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ahmed Yahya Abdulwakil (65) kufariki dunia mwezi April 2024.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , ,

Comments are closed.