KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu

Filed in Michezo by on 21/04/2024 0 Comments

MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu

MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu

MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu

MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumu, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema kupoteza tena mbele ya Yanga kumezidi kufanya safari ya Ubingwa kuwa ngumu.

Akizungumza baada ya dakika 90 za mchezo wa Derby ya Dar Es Salaam ama Kariakoo Derby kumalizika, Matola amekiri kuwa wamepoteza nafasi ya ushindani kuwania ubingwa msimu huu, lakini haina maana kwamba ndio mwisho wa msimu kwani bado wana mechi nyingine zilizobaki.

“Tulianza bila Mshambuliaji, lakini mara baada ya kufungwa mabao mawili, tukamuingiza Mshambuliaji ambaye amefunga bao la kufutia machozi,” amesema na kuongeza;

“Mabadiliko ya mapema pia tuliyoyafanya yametugharimu kwa sababu Mchezaji aliyeingia kafanya makosa, wapinzani wakapata faida ya penalti kutokana na kosa alilolifanya ndani ya 18.”

Matola amesema walikuwa wanatambua jeraha alilokuwanalo, Henock Inonga na waliamini ataweza kumaliza dakika 90, lakini mambo yameenda tofauti, huku akiweka wazi kuwa, beki huyo kapata jeraha jipya.

Inonga alilazimika kufanyiwa mabadiliko dakika ya 12 na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Kazi ambaye muda mchache tangu kuingia kwake, akasababisha penalti iliyokwenda kufungwa na Stephanie Aziz Ki.

MATOLA Akiri Ubingwa Simba ni ngumuKatika hatua nyingine, Matola amezungumzia namna timu yao ilivyo na makosa katika eneo la Ushambuliaji sambamba na ulinzi ambapo wameruhusu mabao kwenye kila mchezo.

“Tatizo la Washambuliaji na Wachezaji wanaopewa nafasi ya kucheza wamekuwa wakishindwa kutumia nafasi sawa na Mabeki makosa yamekuwa yakijirudia na sisi hilo tumeliona tutaenda kulifanyia kazi,” alisema Matola.

 

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *