MBWANA Makata na Soka la Mwanza ni Damu Damu
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MBWANA Makata na Soka la Mwanza ni Damu Damu
MBWANA Makata na Soka la Mwanza ni Damu Damu,Kocha Mbwana Makata ana mchango mkubwa katika Soka la Mwanza ambayo watu wengi hawajui.
Kwa taarifa yako Mbwana Makata amefanya mambo makubwa katika Mkoa wa Mwanza katika medani ya soka kuliko hata mikoa mingine Tanzania.
Makata ameandika historia ya kuipandisha timu ya Pamba Jiji ligi kuu. Timu ambayo imepamba takribani miaka 23 bila mafanikio hayo.
Anakuwa kocha wa kwanza kuweka historia hiyo ingawa pia amelitumikia Soka katika Vilabu vingine vya Mkoa wa Mwanza kwa mafanikio makubwa.
Hiki ndicho alichokifanya Mbwana Makata katika soka la Mwanza.
– 2004 – 2006 alikuwa Nyambiti Ngudu
– 2007 – 2009 Toto African 2008
– Timu ya Mkoa wa Mwanza Robo Finali Taifa Cup
– 2017 – 2018 Alliance Ligi Kuu
– 2023 – 2024 Pamba Jiji Ligi Kuu.
Hii ni historia iliyotukuka na yenye mashiko kwa kila anayefahamu Mbwana Makata.
Anaweza kuwa na madhaifu yake kama binadamu ila ukiangalia mazuri na madhaifu, mazuri ni mengi kuliko madhaifu.
Mbwana Makata anastahili kupongezwa kwa kazi kubwa aliyoifanya, sambamba na kupewa heshima anayostahili.
Kukaa miaka 23 bila Pamba Kupanda Ligi Kuu yeye amefanya kwa msimu mmoja tu.
Aidha Kurejea Ligi Kuu Kwa Pamba Jiji FC kunamfanya kocha Mbwana Makata kuweka rekodi ya kuwa kocha pekee Tanzania ambaye amezipandisha daraja timu nne ndani ya misimu saba.
Alianza na Alliance FC msimu wa 2017/18, Polisi Tanzania FC 2018/19, Dodoma Jiji FC 2019/20 na Pamba Jiji FC 2023/24 huku akitafuna mfupa mgumu ambao uliwashinda makocha wengi kwa zaidi ya miaka 20 kuipandisha Pamba Jiji FC.