RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MFAHAMU Francois Regis CEO Mpya Simba SC

Filed in Michezo by on 27/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

MFAHAMU Francois Regis CEO Mpya Simba SC

MFAHAMU Francois Regis CEO Mpya Simba SC

MFAHAMU Francois Regis CEO Mpya Simba SC

MFAHAMU Francois Regis CEO Mpya Simba SC, Klabu ya Simba imetambulisha rasmi, Francois Regis kutoka Rwanda kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo akirithi mikoba ya Imani Kajula anayemaliza Mkataba wake mwishoni mwa mwezi huu July 2024.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya wakurugenzi ya Simba chini ya Mwenyekiti Mohammed Dewji leo Julai 26, 2024 imefafanua kuwa Regis ataanza kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Agosti 01,2024.

“Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Imani Kajula, kwa niaba yangu na kwa niaba ya Bodi. Mchango wa thamani wa Imani kwa Simba unaacha alama chanya za maendeleo na mafanikio, ambayo yatakuwa ya juu zaidi kutoka ambapo Simba itaendelea kukua,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Simba

MFAHAMU Francois Regis CEO Mpya Simba SC.

Francois Regis taarifa za Wasifu wake zinaonyesha kuwa ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika uongozi wa michezo na hasa soka.

Francois Regis amewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Soka Rwanda kwa zaidi ya miaka mitatu na amekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya APR na pia amewahi kuwa Mratibu Mkuu wa mechi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Francois Regis ni miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha Makocha wa Soka Rwanda ambacho amewahi kuwa Makamu wake wa rais.

Regis pia ana taaluma ya ukocha wa soka akiwa na Leseni ngazi B ya umoja wa vyama vya mpira wa miguu Ulaya (UEFA) aliyoipata chini Ujerumani.

Ni Mtaalam wa masuala ya utawala wa Biashara akiwa na Elimu ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters) na pia ana cheti cha kimataifa cha utunzaji Fedha za umma (IPSAS).

Pia amewahi kufanya kazi kama Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Rwanda, Mkurugenzi wa utawala na Fedha na pia Mkurugenzi wa Uendeshaji wa taasisi tofauti nchini Rwanda.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.