MICHUANO ya Fahari Super Cup 2024 Kufanyika Mwanza
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MICHUANO ya Fahari Super Cup 2024 Kufanyika Mwanza
MICHUANO ya Fahari Super Cup 2024 Kufanyika Mwanza, Mashindano ya Fahari Super Cup 2024 msimu wa tano yanatarajiwa kuanza tarehe 14 Juni 2024 katika uwanja wa Red Cross Ngomeni Kisesa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, yakishirikisha timu 16.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu Mkuu wa Mashindano hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mweta Sports Center, Wilbert Mweta amesema kwa msimu huu wa tano wamefanya Maboresho zaidi ili kuongeza ladha na Ushindani mkubwa kwa timu Shiriki.
Mweta amesema kuwa msimu msimu huu wa 2024 Kuna ongezeko la timu 8 na zile za msimu uliopita 8 hivyo kufanya kuwa timu 16 ambazo zitachuana kutafuta ushindi katika Mashindano hayo ambayo yameongezewa ubunifu zaidi.
Mweta ametaja Faida za Michuano hiyo ambayo itaanza Ijumaa wiki hii kuwa ni kuwaleta pamoja vijana wenye vipaji kutoka timu shiriki kutengeneza wachezaji kwenda kwenye soka la Ushindani Ligi Mbalimbali.
Aidha Mweta amesema kuwa utaratibu wa Mashindano hayo utakuwa wa mechi ya nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasogea mbele kwenye hatua inayofuata.
Kwa upande wa zawadi Mweta amesema kuwa Mshindi wa kwanza anatarajiwa Kuchukua kombe, Medali na Shilingi 1,000,000 huku Mshindi wa pili akipatiwa Medali na Shilingi 500,000.
Pia kutakuwepo na zawadi kwa Kipa Bora na Mfungaji Bora ambapo watapata Shilingi 100,000 kila mmoja.