MOTSEPE Bao la Azizi Ki lilikuwa halali
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MOTSEPE Bao la Azizi Ki lilikuwa halali
MOTSEPE Bao la Azizi Ki lilikuwa halali, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema kuwa bao la Yanga lililokataliwa na Refa Dahane Beida wa Mauritania kwenye mchezo wa Marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika April 06-2024, kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, Afrika Kusini lilikuwa halali.
“Baada ya mchezo wa Mamelodi dhidi ya Yanga nilimwambia Rais Karia ‘nilidhani lile ni goli’ kama Rais wa CAF sikutakiwa kusema chochote. Lakini mnajua, na napaswa kuheshemu mchakato na taratibu zote, lakini kama shabiki wa mpira nilivyoangalia niliona ni goli,”.
“Lakini tunatakiwa kufuata na kuheshimu sheria na VAR lakini nadhani jambo kubwa ni mashabiki kujiamiani tunawahakikishia kuwa Waamuzi, VAR ni ‘WELL CLASS’ na tunahakikisha tumeweka fedha nyingi,” amesema Rais wa CAF, Patrice Motsepe, raia wa Afrika Kusini.
Yanga SC ilitupwa nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns kwa penalti 3-2 kufuatia sare za 0-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam March 30 na ugenini April 06-2024.