MOUSSA Camara Golikipa Mpya wa Simba 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
MOUSSA Camara Golikipa Mpya wa Simba 2024
MOUSSA Camara Golikipa Mpya wa Simba 2024,Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa golikipa, Moussa Camara Kutoka Horoya Horoya Athletic Club ya kwao Guinea.
Moussa Camara mwenye umri wa miaka 25 tayari amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomfanya aitumikie Simba SC hadi 2026.
Hiyo ni baada ya aliyekuwa golikipa tegemeo wa Simba, Ayoub Lakred kupata majeraha yatakayomfanya akae nje ya dimba takribani miezi miwili.
Moussa Camara mzaliwa wa Siguiri, Guinea anakuwa Mchezaji wa 15 kusajiliwa na Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi wa 2024/2025 baada ya kukamilisha usajili wa Wachezaji wengine ambao ni;
Awesu Awesu kutoka KMC FC, Kelvin Kijili kutoka Singida Fountain Gate, Yusuph Kagoma Kutoka Singida Fountain Gate, Karaboue Chamou Kutoka Racing Club d’ Abidjan ya Ivory Coast, Valentin Nouma kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo, Omary Omary Kutoka Mashujaa FC, Debora Fernandes Mavambo Kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Augustine Okejepha Kutoka Rivers United ya Nigeria na Valentino Mashaka Kutoka Geita Gold FC.
Wengine ni Abdulrazack Mohamed Hamza kutoka Super Sport ya Afrika Kusini, Lameck Lawi kutoka Coastal Union, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos, Steven Mukwala kutoka Asante Kotoko na Jean Charles Ahoua kutoka Stella Club d’Adjamé.