MRITHI wa Benchikha Simba huyu hapa
MRITHI wa Benchikha Simba huyu hapa
MRITHI wa Benchikha Simba huyu hapa, Klabu ya Simba ipo kwenye Mazungumzo ya mwisho na Kocha Steve Komphela mwenye umri wa miaka 56 kutoka Afrika Kusini ili arithi mikoba ya iliyoachwa na Kocha Abdelhack Benchikha.
Kama kila kitu kitaenda sawa basi Komphela atatambulishwa kuwa kocha Mkuu wa Simba kwa msimu ujao wa 2024/2025, licha ya kupingwa na baadhi ya viongozi wa juu wa timu lakini anaonekana kuwa na nafasi kubwa.
Komphela ni mzoefu wa soka la Afrika kwani azifundisha timu mbalimbali tangu 2002, lakini kubwa zaidi ni Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana.
Msimu uliomalizika alikuwa na Lamontville Golden Arrows iliyomaliza nafasi ya tisa kwenye Msimamo wa Ligi Kuu nchini Afrika Kusini (South African Premier Division 2023-2024).
Hata hivyo, kama atakuwa yeye au mwingine kuna mambo yanayomsubiri kocha mpya ndani ya Simba iwapo atakabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho ambacho kilimaliza ligi chini ya kocha wa muda Juma Mgunda.
Kama Komphela ataajiriwa Simba au kocha mwingine, moja kazi atakayokuwa nayo kwenye kikosi hicho ni kutengeneza timu mpya kabisa.
Hii ina maana sehemu kubwa ya wachezaji wa Simba wataondoka baada ya baadhi kumaliza mikataba, lakini wengine wataachwa au kuuzwa, kutokana na wachezaji wengi msimu uliopita kuonekana kuwa chini ya kiwango hali ilyochangia timu hiyo ikose matokeo mazuri kwenye mechi zake.
Uongozi wa timu hiyo tayari umeshasema kuwa kuna wachezaji wataondoka na hivi karibuni watatangazwa pia wapya nao watatangazwa.
Hapo kocha mkuu atakuwa na kazi ya kuijenga timu hiyo upya bila kujali wachezaji atakaowasajili yeye ama atakaowakuta.
Tags: MRITHI wa Benchikha Simba huyu hapa, Steve Komphela atajwa Simba, Steve Komphela Kumrithi Benchikha Simba, Steve Komphela Simba SC.