RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


MUONGOZO wa Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Filed in Makala by on 20/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

MUONGOZO wa Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

MUONGOZO wa Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Mfumo wa Vibali vya Kusafiri ni mfumo wa kimtandao unaojiendesha wenyewe (otomati) uliotengenezwa kwaajili ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Kwa kutumia mfumo huu waajiriwa wa Serikali na watumishi wote wa umma wataweza kuomba kibali cha kusafiri nje
ya nchi kwa safari binafsi au za kikazi kwa mtu binafsi au kikundi.

KUFIKIA MFUMO HUU
Ili kufikia mfumo huu:

  • Fungua kivinjari cha mtandao kama vile Google Chrome, Mozilla, Firefox, Safari, Opera Mini, Edge, Internet Explorer n.k.
  • Kwenye eneo la anwani andika anuani ifuatayo http://safiri.gov.go.tz na kikusa kifuatacho kitaonekana:

Jinsi ya kuingia kwenye mfumo
Watumiaji wote wa mfumo wanatakiwa kuingia kwa kutumia jina tumizi na nywila zinazotumiwa katika anwani rasmi za barua pepe za mawasiliano Serikalini. Kuweza kuingia kwenye mfumo;

  • Andika anwani yako ya barua pepe sehemu yenye neno Jina tumizi
  • Andika Nywila yako sehemu yenye neno nywila
  • Bofya Ingia

Kuseti Upya Nywila
Ikiwa umesahau nywila yako, bofya kiungo (link) Umesahau Nywila? na mfumo utakupeleka kwenye skrini ifuatayo ya kuseti upya nywila, halafu utaingiza anwani yako ya barua pepe na namba ya utambulisho.

  • Mfumo utakupelekea kiungo kwa kupata tena nywila yako kupitia anwani yako ya barua pepe.
  • Fungua kiungo na ingiza nywila yako mpya.
  • Rudi kwenye skrini ya kuingia, ingiza utambulisho wako mpya na mfumo utakupeleka kwenye dashibodi husika

DASHIBODI
Dashibodi ya mfumo inaonwa na kila mtumiaji anayefikia mfumo lakini watumiaji wengine hawawezi kuona wanachokiona watumiaji wenzao! Ina maana watumiaji wanafikia taarifa zinazowahusu tu.

Hivi ndivyo dashibodi inatakiwa kuonekana:

Mfumo utajaza baadhi ya taarifa zako binafsi.

  • Chagua aina ya safari kama ni mtu binafsi au kikundi.
  • Ukichagua safari ya kikundi, unatakiwa kuchagua kikundi kimojawapo ambacho umepangiwa, halafu bofya mbele kuendelea.
  • Kama umechagua Safari Binafsi basi bofya inayofuata.
  • Kwenye sehemu ya Maelezo ya Maombi, hakikisha umeingiza namba sahihi ya pasipoti halafu bofya inayofuata, na nyuga nyingine zitajazwa moja kwa moja na mfumo.
  • Kwenye sehemu ya Maelezo ya Safari (Jedwali 3.1) unatakiwa kuchagua mwisho wa safari na kundi la taasisi inayofadhili gharama za safari yako.

  • Ukichagua Taasisi inayogharamia safari kama vile Serikali kwenye herufi A Jedwali 3.1 hapo juu inavyoonyesha, utatakiwa uchague taasisi ya Serikali kwenye herufi B; ukichagua Mfadhili kwenye A, mfumo utakutaka uchague Mfadhili kutoka katika orodha yenye herufi C.
  • Kama gharama za safari yako zinalipwa na Serikali na wafadhili wengine, chagua Mfadhili na Serikali kwenye orodha ya alama A na mfumo utakupa uchaguzi kulingana na upendeleo wako.
  • Kama huoni taasisi kwenye orodha iliyotolewa, chagua nyingine kwenye mojawapo kati ya A, B na C, mfumo utakupa uga wa kujaza taasisi inayolipa gharama zako.
  • Kwa safari unazojilipia, chagua Malipo Binafsi kwenye uchaguzi wa alama A.

Mwisho chagua madhumuni ya safari yako.

Kwenye sehemu ya Gharama za safari, ingiza jumla ya gharama zote zilizooneshwa, kama hujapatiwa gharama zozote zilizooneshwa kwenye nyuga hapa chini, tafadhali weka 0.
Bofya mbele kuendelea.

Kwenye sehemu ya mwisho yenye neno Wasilisha (Jedwali 3.3), andika maelezo mafupi (si zaidi ya maneno 100) ya manufaa ya safari yako kwa taifa.

Kwenye boksi la uchaguzi (Choose File) weka nyaraka kutoka katika hazina yako ya Data kulingana na aina ya nyaraka uliyochagua katika Uga ya pakia nyaraka. Ukitaka kuongeza hati zaidi bofya alama ya kujumlisha (+) au ya kutoa (-) kuondoa baadhi ya hati.

Weka alama kwenye boksi-hakiki kukubali masharti ya kibali cha safari na mwisho bofya kibonye cha Wasilisha kuwasilisha.

ANGALIZO: Baada ya kuwasilisha ombi lako, mfumo utapeleka ombi hilo kwa ofisa anayehusika kwa mapendekezo au idhini na ujulisho huo wa barua pepe utapelekwa pia kwa mtendaji anayefuata.

Kufuatilia ombi la kibali
Mtumiaji yeyote anaweza kufuatilia kujua hadhi ya ombi; kufanya hivyo nenda upande wa kushoto wa menyu, chagua Kibali cha Kusafiri Kufuatilia Ombi

Kuamilisha kibali
Chagua ombi mahususi la kibali kutoka orodha ya vibali Vilivyoidhishwa au Kukataliwa, bofya kibonye kuamilisha na andika sababu za hatua yako.

KUSHUGHULIKIA VIBALI VYA KUSAFIRI (Kwa maofisa wa juu tu)
Maombi ya kibali cha kusafiri yatashughulikiwa na maofisa walioidhinishwa tu, ndio kusema
wasimamizi, Wakuu wa Taasisi, Maofisa Watendaji Wakuu, Makatibu Wakuu na Mawaziri, Msajili wa Hazina na Katibu Mkuu Kiongozi au watu binafsi walioteuliwa na mamlaka fulani.

Mwombaji panapopeleka ombi, Watendaji hao (waliotajwa hapo juu) wataona kikusa kama ilivyo jedwali 4.0 hapa chini.

Bofya inayoingia upande wa kushoto wa menyu au dashibodi, orodha ya maombi mapya itaonekana kama inavyooneshwa kwenye Jedwali 4.0.

Chagua kibali unachotaka kushughulikia kwenye orodha na kitafunguka kukupa paneli kwa pendekezo/idhini au hatua nyingine yoyote ya kuchukuliwa kuhusu kibali. Angalia Jedwali 4.1 kuona paneli ya vilivyoidhinishwa inavyoonekana.

Chagua uamuzi kwenye boksi la uchaguzi (ikiwa utachagua Rudisha, kibali kinarudi hatua iliyopita, kama utachagua Inasubiri, ombi la kibali litasimama na kusubiri hatua zaidi)

Andika sababu kwenye Boksi la sababu kwa hatua yoyote utakayochukua.

Bofya kibonye cha Wasilisha kuwasilisha/kuhifadhi kibali.

KUUNDA KIKUNDI KWA KIBALI CHA KUSAFIRI
Kibali cha Kusafiri Kikundi huundwa na Utawala au Maofisa Rasilimali watu wa taasisi inayotumia mfumo huu. Kuunda Kikundi kwa Kibali cha Kusafiri:

Nenda Kibali cha Kusafri upande wa kushoto wa menyu na bofya Kibali cha Kikundi kama inavyooneshwa kwenye Jedwali 5.0 hapa chini.

Bofya kibonye cha Ongeza Kikundi kilichoko upande wa kushoto juu ya orodha ya vikundi kama inavyooneshwa kwenye Jedwali 4.0 (Ombi la Kikundi) hapo juu.

Baada ya hatua 2, fomu ifuatayo hapa chini itajitokeza ikiwa imejazwa kiotomati maelezo ya Taasisi na ya Mwombaji.

Nenda sehemu ya 3 iliyoandikwa Maelezo ya Safari, ingiza data yote muhimu halafu bofya inayofuata kuona sehemu ya mwisho (Maelezo ya Kikundi).

Kwenye sehemu ya mwisho iliyooneshwa kwenye jedwali hapo juu, ingiza jina la kikundi, idadi ya wafanyakazi watakaokuwa kwenye hiyo safari na hati zinazohusiana na safari hiyo.

Bofya kibonye cha Wasilisha kuhifadhi kikundi kinachosafiri.

Kuongeza Watu Wengine Kwenye Kikundi Baada ya kuunda kikundi , bofya kibonye mbele ya kikundi chochote kilichoundwa na kikusa cha Kuongeza Watu Wengine kitajitokeza.

Chagua taasisi anayotoka mtu huyo.
Chagua mtu huyo kutoka orodha inayoitwa Jina la Mtumiaji.
Bofya Ongeza kuhifadhi.

Serikali imeweka Mfumo wa utoaji Vibali vya kusafiria nje ya Nchi kwa njia ya Mtandao ili kurahisisha na kuongeza ufanisi katika kushughulikia maombi ya Vibali.

Kipengele cha dharura kimewekwa kwa ajili ya safari za dharura tu ili kukidhi maombi ya wagonjwa pamoja na mialiko/safari za kiserikali za dharura.

Hivyo, waombaji wanapaswa kutuma maombi yao siku 14 kabla ya safari zao za kawaida ikiwa ni muda wa chini kabisa. Pia waidhinishaji wa maombi ya Vibali mnakumbushwa kutoidhinisha maombi ya yanayoletwa kwa mlengo wa dharura pasipo kuwa na udharura wa safari husika.

Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi bonyeza hapa kuingia

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.