MWIMBAJI Marco Joseph Bukuru Afariki Dunia
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Marco Joseph Kutoka kundi maarufu la nyimbo za injili la Zabron Singers amefariki Dunia.
Marco alifariki juzi Jumatano wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya kitaifa ya Muhimbili.
Mwimbaji huyo aliripotiwa kuugua uugonjwa wa moyo wiki moja iliyopita, hali iliyomlazimu kurejea nchini kwaajili ya matibabu zaidi akitokea nchini Kenya ambapo kundi hilo lilikuwa kwa ziara.
Baada ya kurejea nchini Marco alipelekwa Hospital ya Bugando ambapo alipatiwa Rufaa ya kwenda Muhimbili ambapo alitakiwa kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo la moyo.
Dada Mkubwa wa Kundi hilo alisema kuwa, Marco alianza kupata ugumu wa kupumua takriban wiki moja iliyopita wakati wa safarini kuelekea Kenya ambapo baada ya vipimo alitakiwa kurejea nchini Kwa matababu zaidi.
Kundi la Zabron Singers kupitia Mitandao ya Kijamii walithibisha kifo Cha Marco Joseph Bukuru Kwa kuandika;
Ni kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Marco Joseph Bukuru, ambaye aliondoka duniani tarehe 21 Agosti 2024. Alikuwa mume mpendwa, baba, kaka, na mmoja wa wahudumu wa Zabron Singers. Familia yetu inakushukuru kwa upendo wako mwingi, sala na msaada katika wakati huu mgumu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Marco Joseph Bukuru alizaliwa tarehe 12/6/1994 na amefariki tarehe 21/8/2024.