MWONGOZO wa Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Mwongozo huu wa Uchaguzi wa viongozi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa umeandaliwa kwa lengo la kufafanua kwa lugha rahisi maudhui ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi za msingi.
Kwa mujibu wa mwongozo huu ngazi za msingi za Serikali za mitaa zina maana ya Mitaa katika
Mamlaka za Miji, Vijiji na Vitongoji katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji zenye Vijiji na Vitongoji.
Kwa kufafanua kwa lugha rahisi mwongozo huu utawasaidia, Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi, Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi na Wadau wengine wa Uchaguzi kufahamu majukumu yao katika kusimamia mchakato mzima wa Uchaguzi.
Aidha, Mwongozo huu utawawezesha wadau wa Uchaguzi, pamoja na mambo mengine, kufahamu haki na wajibu wa vyama vya siasa na wapiga kura.
Ni mategemeo ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuwa, kupitia Mwongozo huu, Uchaguzi utafanyika katika mazingira huru, uwazi, amani na haki kwa washiriki wote. OR – TAMISEMI
kama Mamlaka ya Uchaguzi inatarajia kuwa Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi, Wasimamizi wa Vituo, Mawakala na Wadau wengine wote wa Uchaguzi watashiriki katika
shughuli za Uchaguzi wakizingatia maslahi mapana ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kudumisha demokrasia na kuimarisha amani, utulivu, mshikamano na umoja wa kitaifa.
Pamoja na kufafanua Kanuni za Uchaguzi kwa lugha rahisi, Mwongozo huu umejumuisha pia mtiririko wa matukio ya Uchaguzi kuanzia tarehe ya Tangazo la Uchaguzi hadi tarehe ya Uchaguzi.
Ratiba ya Uchaguzi imefanywa kuwa ni sehemu ya Mwongozo huu ili kurahisisha rejea.
MWONGOZO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA NGAZI ZA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA 2024 DOWNLOAD PDF
SOMA NA HII: RATIBA ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024