RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

MWONGOZO wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada 2023/2024

Filed in Ajira by on 21/11/2023 0 Comments

MWONGOZO wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada 2023/2024

MWONGOZO wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada 2023/2024, FOMU Ya kuomba Mkopo HESLB, Mwisho wa Kuomba Mkopo 2023, Jinsi ya kuomba mkopo kwa wanafunzi wa diploma, MIKOPO vyuo vya kati 2023, Jinsi ya kuomba mkopo Online.

MWONGOZO wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada 2023/2024

MWONGOZO wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada 2023/2024, FOMU Ya kuomba Mkopo HESLB, Mwisho wa Kuomba Mkopo 2023, Jinsi ya kuomba mkopo kwa wanafunzi wa diploma, MIKOPO vyuo vya kati 2023, Jinsi ya kuomba mkopo Online.

Kwa ngazi ya Waombaji wote wa mikopo ya Elimu kwa ngazi ya Stashahada kwa mwaka wa masomo 2023/2024 wanafahamishwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

 • Kusoma na kufuata taratibu za Maombi katika Mwongozo wa mwaka wa masomo 2023/2024;
 • Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne atakayoitumia mwombaji iwe sawa na atakayoombea udahili wa chuo;
 • Kuhakikisha kuwa nyaraka zote za maombi ya mkopo anazowasilisha mwombaji ziwe zimehakikiwa na mamlaka husika;
 • Waombaji wajaze fomu zao kwa ukamilifu na kuzisaini kabla ya kuziwasilisha HESLB kwa njia ya mtandao;
 • Kuhakikisha kwamba vyeti vya kuzaliwa/vifo vimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali wa nyaraka hizo;
 • Kwa mwombaji mwenye taarifa zake za benki ajaze kwa usahihi kwenye fomu ya maombi ya mkopo;
 • kwa mwombaji mwenye Namba ya simu na kitambulisho cha taifa (NIDA) ahakikishe anajaza namba hizo wakati wa kuomba mkopo.
 • Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.

KUFUNGULIWA DIRISHA LA MAOMBI

 • Kwa wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo ya Elimu kwa ngazi ya Stashahada, dirisha la maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 litafunguliwa kuanzia tarehe 07 Oktoba, 2023 hadi tarehe 19 Oktoba, 2023.

SIFA STAHIKI

Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo zinaainisha sifa na vigezo vya jumla kwa wanafunzi wanaohitaji mkopo baada ya kudahiliwa na vyuo vyenye ithibati.

Mwombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

Vigezo vya Msingi vya Mwombaji Mkopo

 • Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 27 wakati wa kuomba mkopo;
 • Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu inayotoa elimu ya ngazi ya kati nchini;
 • Awe amekamilisha na kuwasilisha maombi ya mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS);
 • Asiwe na ajira au mkataba wa kazi wa serikalini au sekta binafsi unaompatia mshahara au kipato;
  DUCA
 • Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (CSEE), Cheti (astashahada) au kidato cha sita (ACSEE) au ndani ya miaka mitano; yaani kati ya mwaka 2019 hadi 2023.

Hali ya Kijamii na Kiuchumi

 • Uyatima; aliyefiwa na mzazi au wazazi
 • Familia au kaya ya kipato duni inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi nyingine za kitaifa zinazotoa ufadhili kwa kaya zenye vipato duni;
  IER
 • Ulemavu wa mwombaji au wazazi wake.

UPANGAJI WA MIKOPO

Upangaji wa mikopo utazingatia vipaumbele vifuatavyo:-

 • Mwanafunzi mwenye udahili kwenye programu za vipaumbele vya Taifa kama zilivyofafanuliwa katika Kipengele cha 6 cha Mwongozo huu zitazingatiwa;
 • Ufaulu wa kitaaluma uliomuwezesha kudahiliwa kwa ajili ya elimu ya ngazi ya kati;
  na
 • Hali ya kijamii kama ilivyofafanuliwa katika kipengele cha 3.2 cha mwongozo huu.

NYARAKA ZA KUAMBATISHA WAKATI WA MAOMBI YA MKOPO

Zifuatazo ni nyaraka muhimu za kuambatisha kwenye maombi ya mkopo:

 • Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
  itisha uyatima
 • Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au namba ya uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
 • Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji iliyoidhinishwa na
  Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
 • Fomu ya kuthibitisha Ulemavu wa mzazi wa mwombaji iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
 • Namba ya kaya ya Mnufaika kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

MAENEO NA PROGRAMU ZA KIPAUMBELE KATIKA UTOAJI WA MIKOPO

Maeneo ya Kipaumbele
Mkopo utatolewa katika maeneo makuu sita yakiakisi vipaumbele vya Taifa kama ilivyoainishwa katika tangazo la Serikali Namba 715 la tarehe 29 Septemba 2023.

Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-
BOA

 • Afya na Sayansi Shirikishi (‘Health & Allied Sciences’);
 • Elimu ya Ualimu (Education and Teaching’);
 • Uhandisi wa nishati (‘Energy Engineering’);
 • Usafiri na Usafirishaji (Transport & Logistics’);
 • Madini na Sayansi ya ardhi (‘Mining & Earth Science’) na
 • Kilimo na Mifugo (Agriculture & livestock’)

Programu za kipaumbele
Katika mwaka wa masomo 2023/2024 mikopo itatolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika Program/Stashahada zinazoangukia/zilizomo katika maeneo sita ya kipaumbele yaliyoidhinishwa – rejea kipengele 6.

Dirisha La Mkopo 2023 Kufunguliwa lini, Vigezo vya kupata Mkopo ngazi ya diploma PDF, mikopo kwa wanafunzi wa diploma 2023/2024, Mikopo kwa Diploma 2023 PDF, mwongozo wa mkopo 2023/24, Fomu Ya kuomba Mkopo, Vigezo vya kupata mkopo vyuo vya kati.

MWONGOZO wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada 2023/2024 Donwload PDF Kusoma ZAIDI

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *