NACTVET Matokeo ya Uchaguzi wa Awamu ya Pili 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2024/2025 yametangazwa tarehe 18 Agosti, 2024.
Baraza lilifungua dirisha la awamu ya pili kuanzia tarehe 11 Julai hadi tarehe 10 Agosti, 2024 ambapo jumla ya waombaji 20,163 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/ programu walizozipenda.
Aidha, Jumla ya waombaji 3,806 hawakuwa na sifa kwenye programu walizoomba.
Jumla ya waombaji 13,201 wamechaguliwa kujiunga katika vyuo 206 vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi, wanawake ni 6,512 (49.3%) na wanaume ni 6,689 (50.7%). Waombaji 193 walichaguliwa kwenye vyuo 33 vya serikali na waombaji 13,008 katika vyuo 173 visivyo vya serikali.
Aidha, waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu na vyuo walivyoomba wanashauriwa kuomba kujiunga katika programu na vyuo vyenye nafasi katika dirisha la awamu ya tatu kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja.
Waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo ya uchaguzi kupitia tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kwa kubonyeza CAS Selection 2024 kwa ajili ya kupata taarifa zaidi.
Aidha, Baraza linautaarifu umma kuwa dirisha la awamu ya tatu limefunguliwa tarehe 18/08/2024 hadi tarehe 30/08/2024.
Uhakiki Muhula wa Septemba 2024
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NACTVET Matokeo ya Uchaguzi wa Awamu ya Pili 2024/2025