NACTVET Matokeo ya Uhakiki Waliochaguliwa Awamu ya Kwanza Mkupuo wa Septemba 2024/2025
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NACTVET Matokeo ya Uhakiki Waliochaguliwa Awamu ya Kwanza Mkupuo wa Septemba 2024/2025
NACTVET Matokeo ya Uhakiki Waliochaguliwa Awamu ya Kwanza Mkupuo wa Septemba 2024/2025, Baraza linautaarifu umma kuwa matokeo ya uhakiki wa waombaji waliochaguliwa katika awamu ya kwanza kujiunga na vyuo katika programu mbalimbali kwa mkupuo wa Septemba 2024/2025 katika ngazi ya Astashahada na Stashahada yametolewa rasmi leo tarehe 5 Agosti, 2024.
MATOKEO YA UHAKIKI WA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA AWAMU YA KWANZA MKUPUO WA SEPTEMBA 2024/2025
Jumla ya waombaji 31,523 wanawake wakiwa ni 15,012 (46.9%) na wanaume
16,732 (53.1%) waliwasilishwa na vyuo kwaajili ya uhakiki.
Kati yao, jumla ya waombaji 31,056 (98.5%) wanawake 14,804 na wanaume 16,252 wamekidhi vigezo na sifa za kujiunga na programu walizochaguliwa.
Waombaji 467(1.5%) hawakuwa na sifa katika programu walizochagua.
Waombaji wote wanaweza kupata taarifa zao za uhakiki kwa kutumia msimbo uliotumwa kwenye namba ya simu, kwa kubonyeza kitufe cha “Uhakiki muhula wa Septemba 2024” katika tovuti ya Baraza www.nactvet.go.tz.
Baraza linawasisitiza waombaji wote kutunza msimbo waliotumiwa kwani ndio utatumika katika usajili pindi mwombaji atakapofika chuoni kwaajili ya kuanza masomo.
Aidha, Baraza linavielekeza vyuo kuwasajili waombaji waliohakikiwa na Baraza na wenye sifa watakaofika chuoni kuanzia tarehe 7 Oktoba hadi 30 Novemba, 2024.
Usajili utafanyika kwa kutumia msimbo uliotumwa na Baraza kwenye namba ya simu ya mwombaji.
Chuo kitakachokiuka taratibu za udahili, hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya chuo husika.
Aidha Baraza limefungua dirisha la pili kuanzia tarehe 5 Agosti hadi 18 Septemba, 2024 ili waombaji waliohakikiwa na kuonekana kuwa hawakukidhi vigezo kwenye programu walizoomba kuweza kuomba programu wanazokidhi vigezo kwenye dirisha hili; na ambao hawakuomba katika awamu ya kwanza kuweza kufanya maombi katika awamu hii.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD TANGAZO UHAKIKI SEPTEMBER INTAKE 2024 FINAL – NIJUZEHABARI.COM
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NACTVET Matokeo ya Uhakiki Waliochaguliwa Awamu ya Kwanza Mkupuo wa Septemba 2024/2025