NAFASI 10 za Kazi Kampuni ya Mabasi RATCO
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Kampuni ya RATCO LIMITED inayojishughulisha na usafirishaji wa abiria na mizigo inatangaza nafasi za kazi katika kada zifuatazo:-
✅KONDAKTA NAFASI SITA (6)
✅FUNDI MSAIDIZI (TINGO) NAFASI (4)
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI YA KONDAKTA:-
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na elimu kuanzia kidato cha nne 4 na kuendelea.
- Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
- Ambaya amesoma taaluma ya uhudumu wa abiria (NIT) atapewa kipaumbele.
- Ambaye hajawahi kupatikana na makosa ya jinai.
MAJUKUMU
Kuhudumia abiria katika maeneo ya ofisi na ndani ya basi Usafi wa basi na maeneo yote
Kukusanya fedha nauli kwa abiria na mizigo na kuwasilisha kwa mhusika Kuandaa taarifa ya makusanyo ya fedha akiwa safarini.
SIFA ZA MWOMBAJI FUNDI MSAIDIZI (TANBOY)
- Awe na taaluma ya ufundi wa magari
- Awe na uzoefu wa miaka miwili (2) katika taaluma hiyo
- Ambaye hajawahi kupatikana na makosa ya jinai.
- Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 35.
MAJUKUMU
- Kusaidia majukumu ya ufundi safarini na garage
- Kusaidia kutoa ushauri wa kiufundi.
- Kuhudumia abiria anapokua safarini
Barua ya maombi iambatanishwe na utambulisho kutoka Serikali ya mtaa pamoja na barua za wadhamini wawili ambao wamethibitishwa na Serikali ya mtaa.
Maombi na wasifu (CV) yawasilishwe kwa mkono kuanzia tarehe 29/08/2024 katika ofisi za RATCO Tanga, zilizopo jirani na uwanja Mkwakwani, Magomeni na Lumumba Dar es salaam au tuma kwa barua pepe: ratcolimited@gmail.com
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05.09.2024 saa 10:00 jioni.