RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Bagamoyo July 14-2024

Filed in Ajira by on 14/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Bagamoyo July 14-2024

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Bagamoyo July 14-2024

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Bagamoyo July 14-2024

NAFASI 10 za Kazi Wilaya ya Bagamoyo July 14-2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri` ya Wilaya ya Bagamoyo amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka
kwa Katibu Mkuu OR-Utumishi chenye Kumb. Na. FA.97/200/01/09 cha tarehe 25/06/2024.

Hivyo anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada mbili (02) kama
zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO 15-07-2024

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA DARAJA II – NAFASI TANO (5).

SIFA ZA MWOMBAJI.
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) ya Uhazili na awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata Progamu ya Kompyuta za Ofisi kama vile Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI.

  • Kuchapa barua, taarifa, nyaraka za kawaida na za siri.
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa.
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake  na ratiba za kazi zingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/ Kitengo/Sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi na
  • Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali TGSC

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II (Records Management Assistant II) Nafasi – 5

SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika Fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa Kompyuta.

KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II.

  • Kutafuta Kumbukumbu/Nyaraka/Mafaili yanayohitajika na wasomaji.
  • Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa Kumbukumbu/Nyaraka.
  • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/Nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya Ofisi.
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika masijala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu/nyaraka.
  • Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
  • Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS C

MASHARTI YA UJUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya
    taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Carriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (Email adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne
    na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika
    kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional
    Certificate from Respective Boards).
  • Waombaji walisoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka
    husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 25 Julai, 2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,
S.L.P 59
BAGAMOYO

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment
Portal”

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.