RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 11 za Kazi Halmashauri ya Mji Newala July 17-2024

Filed in Ajira, Uncategorized by on 17/07/2024

NAFASI 11 za Kazi Halmashauri ya Mji Newala July 17-2024

NAFASI 11 za Kazi Halmashauri ya Mji Newala July 17-2024

NAFASI 11 za Kazi Halmashauri ya Mji Newala July 17-2024

NAFASI 11 za Kazi Halmashauri ya Mji Newala July 17-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri Ya Mji Newala 18-07-2024,Kufuatia Halmashauri ya Mji Newala kupata kibali cha Ajira chenye Kumb. Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024, chenye nafasi ya Dereva Daraja la II (5), Dereva wa Mitambo Daraja la II (1) na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (5) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama zilivyoorodheshwa katika
tangazo hili:-

✅DEREVA DARAJA LA Il – NAFASI 5

MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA DARAJA II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
    Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (log book)
  • Kufanya usafi wa gari.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne na Leseni ya Daraja la C au E ya
uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka
mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya
uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au
NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS B1 kwa mwezi

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 3

MAJUKUMU YA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista
  • Kusambaza majalada kwa watendaji Kupokea
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
  • Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye Shubaka/kabati la majalada au mahali pengine yanapohifadhiwa
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi
  • SIFA ZA MWOMBAJI:
    Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliehitimu mafunzo ya stashahada/ Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masjala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS C1 kwa mwezi.

✅DERAVA WA MITAMBO II (PLANT OPERATOR) – NAFASI MOJA (1)

MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA WA MITAMBO II

  • Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa dereva mitambo mwenye
    uzoefu.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Kidato cha IV ambao wana leseni Daraja la ‘’G’’ ya kuendesha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo, wenye, uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu (300) au miezi mitatu (3) bila kusababisha ajali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali TGOS A kwa Mwezi

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
    Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced
    Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Wakatakao kidhi Sifa zinazotakiwa ndio pekee watakaoitwa katika Usahili.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 29/07/2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Newala,
S.L.P 39
63482 NEWALA

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

Tags:

Comments are closed.