NAFASI 11 za Kazi Wilaya ya Gairo July 13-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 11 za Kazi Wilaya ya Gairo July 13-2024
NAFASI 11 za Kazi Wilaya ya Gairo July 13-2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo amepokea kibali cha Ajira chenye kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GAIRO 13-07-2024
Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi
kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:-
✅DEREVA DARAJA II – NAFASI 01
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
- Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote,
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
- Kufanya usafi wa Gari,
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI)/awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajari.
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi
ya uendshaji magari (basic driving course) inayotolewa na Chuo cha VETA au NIT au chuo kingine kinachotambulika na Serikali..
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 10
KAZI NA MAJUKUMU YA NAFASI ZA MTENDAJI WA KIJIJI
- Afisa Masuhuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B .
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wanaojulikana na kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma.
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 26 Julai, 2024.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayata shughulikiwa. Barua ziandikwe kwenye Anwani ifuatayo;-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo,
S.L.P 40,
GAIRO
DONWLOAD PDF DOCUMENT